2014-06-02 09:00:05

Vita na utekaji nyara wa watu ni mambo yasiyoweza kuvumilika!


Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa Vatican anasema, Kanisa limepokea kwa furaha kubwa kuachiliwa kwa Wamissionari watatu waliokuwa wametekwa nyara tangu mwanzoni mwa Mwezi Aprili na kuachiliwa huru hapo tare 1 Juni 2014. Baba Mtakatifu Francisko aliyekuwa anafuatilia kwa makini tukio hili amehabarishwa kuhusu kuachiliwa kwa Wamissionari hawa na kwamba, Kanisa linamshukuru Mungu kwa tukio hili kuhitimishwa kwa hali ya amani.

Kanisa litaendelea kusali kwa ajili ya kuombea amani na linawataka waamini na watu wote wenye mapenzi mema kusimama kidete kupinga aina zote za matumizi ya nguvu, chuki na vita Barani Afrika na katika nchi nyingine duniani. Bado kuna watu wasiokuwa na hatia wanaendelea kuteseka kutoka na vita pamoja na kinzani za kijamii jambo ambalo kamwe haliwezi kuvumiliwa!







All the contents on this site are copyrighted ©.