Katika Maadhimisho ya Siku kuu ya Bikira Maria kumtembelea Elizabeth, ambayo inaadhimishwa
kila mwaka ifikapo tarehe 31 Mei, Baba Mtakatifu Francisko ametumia fursa hii kufunga
rasmi mwezi uliotengwa na Mama Kanisa kwa ajili ya Ibada kwa Bikira Maria kwa kushiriki
kusali Rozari na waamini waliokuwa wamekusanyika kwenye Bustani za Vatican.
Baba
Mtakatifu anasema, baada ya Bikira Maria kupashwa habari na Malaika kwamba atakuwa
ni Mama wa Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu na habari kuhusu binamu yake Elizabeth
kupata ujauzito, aliondoka haraka kwenda kumhudumia. Ni Mama ambaye yuko tayari kuwasikiliza
na kuwasaidia wale wote wanaokimbilia ulinzi na tunza yake ya kimama. Bikira Maria
ni mama asiyepoteza wakati yuko tayari kuhudumia!