2014-05-31 09:14:33

Ujumbe wa Papa kwa mkutano wa ujenzi wa Madaraja kati ya binadamu na Mungu.


Kwa ajili ya tukio la mkutano Katoliki wa 99 ambao hukutanisha waamini kutoka sehemu zote za Ujerumani na pia Jamhuri ya Czech , Austria na nchi zingine jirani za Ulaya, mkutano unaojulikana kwa jina “Katholikentag” uliofanyika katika mji wa Regensburg, Baba Mtakatifu Francisko amepeleka ujumbe na salam zake za Kibaba kwa washiriki wote wa mkutano huo. Mkutano ulioanza Mei 28 - Juni 1, chini ya kauli mbiu " Kujenga Madaraja pamoja na Kristo. "
Salam za upendo za Baba Mtakatifu zimeelekezwa kwa Maaskofu wote, Mapadre , Mashemasi na wale , kwamba, katika siku hizi ambamo wameweza kuwa na maadhimisho ya pamoja , na kupata fursa ya kujifunza kutoka kwa kila mmoja na kuomba kwa ajili ya kila mmoja, Mkutano huu wa “Katholikentag” , umewawezesha kuishuhudia imani yao kama wajenzi wa madaraja katika kanisa na katika jamii.

Ujumbe wa Papa, umeendelea kusema kwamba, Wakristo, wana kazi ya kuendelea kujenga madaraja ya uhusiano na wengine kwa kufanya mazungumzo juu ya hoja na changamoto za kimaisha hasa bila kupuuza huduma isiyokuwa na mipaka kijamii , kidini au mahusiano ya binadamu .Papa amesisitiza, "Kristo ni msingi wa kuanza kazi hii ya ujenzi wa madaraja na kwa kweli, ni Yeye ndiye aliye mshindi dhidi ya madaraja ya kujitenga kati ya watu na kati ya Mungu na mwanadamu ( Efe 2:14). Na kwa kifo chake juu ya Msalaba na ufufuo wake Yeye alijenga daraja kwa ajili yetu na maisha. Na kupaa kwake , Yeye anakuwa daraja la ujenzi kati ya Mungu na binadamu , na kuelekea daraja la kati ya nyakati na milele. Katika Ubatizo na Kipaimara, anatuita kumfuata, kama wajenzi wa daraja”.

Ujumbe wa Papa , unaagalisha katika historia akisema kwamba, historia inatufundisha kuwa mazungumzo ni si kazi rahisi. Na imepita karibia kipindi cha miaka mia tangu kuonekana kwa matokeo hasi ya watu kupuuza majadiliano na kujijengea kuta za utengano ambazo hazikuzaa matunda mazuri. Papa ameeleza kwa kurejea matokeo ya Vita Kuu ya Dunia, iliyokuwa kitisho kikubwa kwa watu. Vita vilivyo fuatiwa na mgogoro mwingine mbaya zaidi wa kutisha wa ndani ya mioyo, ulioongeza kuta za kutoaminiana, chuki na hasira kwa wengine. Hivyo mtu hujitenga mwenyewe katika chuki yake.

Papa anasema, ukuta wa kujitenga huanza kujengwa na mtu mwenyewe . kwanza katika moyo wake na kisha kwa watu wengine na katika nyumba na jamii . Na hivyo inakuwa vigumu kuishi kwa maridhiano ! Papa ameeleza na kutaja mfano hai wa jinsi nchi ya Ujerumani ilivyojenga ukuta ulioleta uchungu na adha kwa watu, ukuta wa Berlin. Kiasi gani ukuta huo ulileta maumivu na mateso! Lakini basi, daima kulikuwa na watu walio kusanyika katika makanisa kuombea amani . Na kwa mujibu wa maombi yaliyo tolewa katika mji huo , wiki baada ya wiki, na watu zaidi na zaidi kujiunga nao, hatimaye , Ukuta wa Berlin uliangushwa. Mwaka huu inatimia miaka 25 ya kusherehekea kuangusha kwa ukuta huo. .Hili linaonyesha utume wa Wakristu katika kusali na kutoka nje kwa ajili ya kupeka kwa wengine Habari Njema, ambamo mna uvuvio wa ubinadamu.
Kujenga madaraja pamoja na Kristo maana yake na juu ya yote ni kuomba. Maombi ni si porojo za mitaani, lakini ni mazungumzo halisi kati ya watu , ambamo Kristo hukutana na sisi na kutusaidia . Lakini ni lazima kuwa makini, kwa sababu wakati mwingine Yesu anazungumza polepole . Yeye anaongea na sisi kwa njia ya Injili na kwa njia ya mikutano yetu na ndugu zetu. Kitu muhimu ni kuwa macho na kusoma Injili mara kwa mara.Ni kutegemea mwongozo wa Bwana na huruma.
Na kwamba Mkutano huu wa “Katholikentag”, unakuwa ni ishara ya mazungumzo ya kweli , kuzungumza pamoja na Kristo na kati ya washiriki katika ujenzi wa madaraja kwa ajili ya amani na wokovu wa milele. Papa alihitimisha ujumbe wake kwa kuwatakia kila la heri kwa mkutano huo na kuwapa baraka zake za baraka kitume.








All the contents on this site are copyrighted ©.