2014-05-31 11:56:25

Papa Francisko kukutana na Catholicos Aram I,wiki ijayo.


Kiongozi wa Kanisa la Kitume la Armenia la Cilicia , Catholikos Aram I, wiki ijayo tangu tarehe 3-6, ana ratiba ya kuzuru Roma, ambamo pia atakutana na Papa Francisko wakati wa Ibada ya Kawaida ya June 5. Ziara ya Catholicos Aram I, hasa ni kukutana na wajumbe wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Kukuza Umoja wa Kikristo , na idara za Curia ya Roma. Na pia atatembelea kaburi la Mtakatifu Petro ndani ya Kanisa Kuu la Vatican, na atatolea sala zake mbele ya sanamu ya Mtakatifu Gregory mwangazaji , iliyoweka upande wa Kaskazini mwa Viwanja wa Vatican.

Catholicos Aram I, alichaguliwa kuliongoza Kanisala Kitume la Armenia na Mkutano Mkuu wa Kanisa hilo , 28 Juni 1995. Na alikutana na Papa Yohana Paulo II mwaka 1997, na pia Papa Benedict XVI mwaka 2008 Novemba 23-27 . Katika mikutano yake miwili na Papa Ratzinger : Novemba 24, waliongoza sala ya kiekumeni katika kanisa dogo la kitume la Mama wa Mkombozi , na kuwa na mkutano wa hadara kwa pamoja Novemba 26.

Kanisa la Kitume la Armenia, lina wafuasi wapatao milioni 6, ikiwa ni pamoja na Wakatoliki wa madhehezu mawili ya Etchmiadzin na Antelias , katika ushirika kamili lakini kila moja likiwa huru katika hatua za utawala wa maoni, na ni wanachama wa Tume ya Pamoja ya Kimataifa ya Mazungumzo ya kiteolojia kati ya Kanisa Katoliki na wawakilishi Makanisa ya Mashariki ya Kiotodosi, na Upatriaki wa Armenia ya Yerusalemu na Armenia ya Constantinople , ambayo hutegemea Etchmiadzin kwa masuala ya kiroho.
Na kati ya Kanisa Katoliki la Ulimwengu na Kanisa la Kitume la Armenia kuna mahusiano mazuri, tangu Mtaguso Mkuu wa pili Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.