Rais Peter Mutharika wa Malawi, Jumamosi tarehe 31 Mei 2014 ameapishwa kuwa Rais wa
Malawi baada ya kutangazwa na Tume ya Uchaguzi nchini Malawi dhidi ya Joyce Banda
aliyekuwa Rais wa Malawi, siku chache zilizopita! Peter Mutharika kabla ya kuapishwa
kuwa Rais wa Malawi alikuwa ni waziri wa mambo ya nchi za nje wa Malawi na kaka yake
Rais Bingu wa Mutharika aliyefariki dunia kunako mwaka 2012.
Katika hotuba
yake ya kwanza kama Rais wa Malawi, Bwana Peter Mutharika amewataka viongozi wote
waliokuwa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea Urais nchini Malawi, kuunganisha nguvu
zao kwa ajili ya umoja na mshikamano wa kitaifa. Rais Joyce Banda amekiri kushindwa
katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 20 Mei 2014. Amempongeza Rais Peter Mutharika
kwa ushindi wake wa "cheee" na kuwataka wananchi wa Malawi kuheshimu maamuzi ya wapiga
kura.
Rais Peter Mutharika ameshinda kwa asilimia 36.4% za kura zote zilizopigwa
ambazo ni sawa na kura millioni 1.9.