2014-05-30 16:02:40

Watakatifu wapya kutangazwa hivi karibuni


Mshereheshaji mkuu wa Ibada za Kipapa, Monsinyo Guido Marini , kwa agizo la Baba Mtakatifu Francisko anatangaza kwamba Alhamisi Juni 12, 2014 , saa 10 asubuhi, katika ukumbi wa Mkutano wa Makadinali ulioko katika jengo la Kitume la Vatican, wakati wa maadhimisho ya Masifu ya adhuhuri , kutafanyika Mkutano wa kawaida, wa Makardinali kwa lengo la mchakato wa kutajwa Wenye Heri wafuatao katika daraja la Watakatifu,
- Giovanni Antonio Farina , askofu wa Vicenza, mwanzilishi wa Shirika la Masista wa Mtakatifu DOROTEA Mabinti wa Mioyo Mitakatifu;
- Chavara Kuriakose Elias la Familia Takatifu , Padre na mwanzilishi wa Usharika wa Carmelites wa Maria asiyekuwa na ndoa ;
- Ludovico da Casoria , Padre wa Shirika la shirika la Ndugu Wadogo , mwanzilishi wa Usharika wa Masista wa Elizabeti Wafransiskani;
- Nicholas Longobardi , wa Shirika la Wamini;
- Eluvathingal Euphrasia ya Moyo Mtakatifu , wa Usharika wa Masista wa Mama wa Karmeli ;
- Amato Ronconi , Mwanashirika wa Kanuni ya atu katika Shirika la Mtakatifu Francis na mwanzilishi wa Hospitali ya Wakimbizi maskini katika eneo la Saludecio, ambako kwa sasa ni nyumba ya mapumziko ya Mwenye Heri Pia Beato Amato Ronconi ."

Makardinali Wakazi wa Rome, siku hiyo wanaombwa kukutana saa 9.30 katika Ukumbi wa Makaridinali ulioko mjini Vatican, wakiwa wamevaa vazi lao rasmi.








All the contents on this site are copyrighted ©.