Mwaliko umetolewa kuwaalika Wakristo ,kutoihama kutoka Nchi Takatifu. Ni wito wa Patriaki
wa Antokia ya Wamaronaiti , Patriaki Bechara Boutros Rai , ambaye katika siku za
karibuni, amekuwa Palestina na Israel, kwa ajili ya kushiriki katika baadhi mambo
muhimu ya Hija ya Papa Francisko katika Nchi Takatifu. Ombi lake kwa Waarabu
Wakristo wa Palestina, alilitoa Jumanne iliyopita, wakati wa Ibada ya Misa, katika
Parokia Katoliki ya Mama yetu wa Fatima ya Beit Sahour , karibu na Bethlehem. "Kaeni
katika nchi yenu , na kukabiliana na changamoto kwa pamoja," alisema Patriaki Rai
na kuwataka kila mtu kukikataa kishawishi cha kutaka kuuza ardhi badala waihifadhi
kwa ajili ya urithi huu wa thamani , hata kwa gharama ya sadaka ."
Siku
ya Jumapili Patriarki Rai alikutana na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas , ambako Patriarki
alipewa kuwa tuzo ya "Nyota ya Yerusalemu" ambayo ni ishara ya heshima ya juu inayotolewa
na Mamlaka ya Palestina, kwa mtu aliyefanya zaidi kulisadia taifa la Palestina. Patriarki
Rai, ametunukiwa heshima hiyo kwa ajili ya ujasiri wake katika kutetea eneo la Nchi
Takatifu , kama ilivyoelezwa katika taarifa iliyotolewa na uwakilishi wa Palestina
nchini Lebanon. “Ni nani hataki amani katika Palestina, " alihoji Patriaki Rai, wakati
akikutana na Rais wa Palestina. NI nani hataki amani Mashariki ya Kati. "
Patriaki
Rai ni kiongozi wa kwanza wa dini mahalia nchini Lebanon na eneo la Israel tangu
mwaka 1948 , mwaka wa kuundwa kwa serikali ya Isralel ya Wayahudi. Lebanon iliionyesha
upinzani wa uamuzi wa Patriki Rai, kuwa na mahusiano na nchi ambayo wao walikuwa
hawajatia saini mkataba wa amani, baada ya migogoro ya miongo kadhaa iliyopita.
Kadi. Rai alitetea sababu ya uchaguzi wake , akisema yeye alitaka kutembelea Nchi
Takatifu kama Mkristo katika eneo hilo lenye kwa na mizizi ya Ukristo. Patriaki
Rai aliyepokea idhini ya kusafiri toka Mamlaka ya Kiraia ya Lebanon, alitembelea
Parokia ya Maronite ya Yopa, Nyumba ya watawa ya Latrun Yerusalemu ya Mashariki na
mwisho wa wiki, ana mpango wa kukutana na jamii ya Lebanon wanaoishi eneo la Galilaya.
Israel inakadiriwa kuwa na Wakristu 11,000 Maronite .