Mkuu wa Ofisi ya habari katika Jimbo Takatifu , Padre Federico Lombardi, Alhamis
alithibitisha kwamba mchana Jumapili ya June 8 , 2014, Rais Shimon Peres wa Israel
na Rais Mahamoud Abbas wa Palestina, wameitikia mwaliko wa Papa Francisko , kushiriki
katika mkutano wa sala Vatican, kwa nia ya kuombea amani.
Papa Francisko,
alitoa mwaliko huu akiwa katika ziara yake ya kitume katika Nchi Takatifu, baada
ya kuogoza sala ya Malkia wa Mbingu, iliyotanguliwa na Ibada ya Misa kaatika Uwanja
wa Hori Takatifu mjini Bethlehemu , Jumapili asubuhi Mei 24 2014. Katika tukio
hili Papa Francisko alisema: ninaitolea nyumba yangu ya mjini Vatican kuwa mahali
kwa ajili ya mkutano huu wa sala. Alisema, Mahali hapa ambako Yesu, Mwana Mfalme
wa amani alizaliwa , ninapenda kuwaalika Rais Mahmoud Abbas, pamoja na Rais Shimon
Peres , kuungana nami kutolea maombi pamoja kwa Mungu, kwa ajili ya zawadi ya amani.
Kukutana kwetu hautakuwa wakati wa majadiliano au maongezi ya kutafuta majadiliano
, lakini ni kutolea sala kwa Mungu. Sisi sote tunapenda kuishi kwa amani . Sisi sote
tunataka amani, alisisitiza Papa ukweli huo, kwamba watu wengi wanapenda kujenga
amani siku hadi siku kupitia ishara ndogo ndogo na vitendo ; wengi wanateseka, na
bado wana subira katika juhudi za kuleta amani . Papa alieleza hasa akiwalenga
viongozi waliowekwa kwa ajili ya huduma kwa watu, kwamba ni wana wajibu wa kuwa
vyombo na wajenzi wa amani , na hasa kupitia sadaka za sala. Papa alionyesha kutambua
kwamba, Ujenzi wa amani si jambo jepesi , lakini yamezekana. Kuishi bila amani ni
adhabu. Papa alitoa pia himizo kwa wote waume na wake wa nchi hizi, na wa dunia
nzima , kila mmoja wao , kuombea amani na kuweka mbele ya Mungu matumaini yao ya
dhati kwa ajili ya amani.