2014-05-30 09:14:58

Papa ateua wajumbe kwa ajili ....


Kati ya shughuli muhimu zilizofanywa na Baba Mtakatifu siku ya Alhamis ni pamoja na kukutana na Mheshimiwa Plamen Oresharski , Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Bulgaria. Na pia alikutana na Mosinyori Francesco Follo , Mtazamaji wa kudumu Shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Elimu , sayansi na Utamaduni UNESCO.

Aidha aliwateua kuwa Wajumbe katika Shirika la Mafundisho ya imani Sadikifu ya Kanisa Katoliki: Katibu wa Jimbo la Papa, Kardinali Pietro Parolin; na Askofu Mkuu Stanislaw Gadecki ya Poznan, Poland, na rais mpya wa Baraza la Maaskofu Poland , Askofu Rudolf Voderholzer na Askofu wa Regensburg, Ujerumani.








All the contents on this site are copyrighted ©.