Ni lazima kusema ukweli : maisha ya Kikristo si lelemama muda wote . Ni vyema kutambua
na kukubaliana kwamba, pia kuna wakati wa kulia na kuteseka, wakati wa kuugua , wakati
wa matatizo ya kifamilia,ya watoto, ya mke, ya mme na hata matatizo ya kiuchumi ,
kuona kwamba mshahara hauwezi kukidhi mahitaji ya familia hadi mwisho wa mwezi,licha
ya kuwa na mtoto au mke au mme mgonjwa. Pengine hata inakuwa vigumu kulipa kodi ya
nyumba au mkopo wa nyumba au matatizo mengine mengi yanayokabili jamii.
Lakini
Yesu anatuambia tusiwe na hofu. Tusiwe watu wa huzuni , au watu wa kulilia tu na
kuhuzunika, ila tuwe watu wa kufurahi tu hata katika matatizo na hata wakati watu
wanapotuudhi au kutochokoza. Ni mahubiri ya Papa Francisko, mapema siku hii ya Ijumaa,wakati
akiongoza Ibada ya Misa katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta la mjini Vatican.
Papa
alikiri kwamba wakati wa matatizo mara nyingi tunalisahau ahadi hii ya Yesu kwmba,
tusiogope. Tunasahau kwamba, mateso ni wakati wa kuwa na furaha kwa sababu ni wakati
wa kujitakasa kwa shuhuida za maisha ya kila siku. "Huzuni yako inarejea kuwa furaha,
ingawa ni vigumu kufurahia wakati unateseka kwa maradhi au kuw ana mtoto mgonjwa".
Lakini Yesu anasema, "jipeni moyo! Haya! Kesho utakuwa na furaha".
Papa alihimiza,
yatupasa kusikiliza wito huu wa Yesu , unaotuondoa katika giza, wakati ambao hatuoni
matumaini yoyote. Na Papa alionyesha imani yake kwa Bwana kwamba, Bwana anao uwezo
wote wa kuigeuza huzuni hii na kuwa furaha . Na kwamba hajui kwa jinsi gani, lakini
anajua ni hivyo. Ni kupitia kitendo cha imani katika Bwana. Tendo la imani !
Daima
kuwa jasiri katika mateso na kufikiri kwamba baadaye, Bwana anakuja kwa furaha
kufuta giza hili la mateso . Bwana aliachia ahadi hii, na sisi sote tunapaswa kuyapokea
yote katika furaha hii, ya matumaini. Na ishara kwamba tuna furaha hii kwa matumaini
ya amani . Wangapi wagonjwa, ambao mwishoni mwa maisha na maumivu, wao sasa wamepumzika
kwa amani kiroho?
Hili linapaswa kuwa mbegu ya furaha yetu , furaha ya
tumaini na amani, Papa alieleza na kuhoji iwapo tuna amani kiroho wakati wa giza,
wakati wa taabu, wakati wa mateso , wakati mgonjwa wetu, ? Je, tuna amani ? Kama
una imani , una mbegu ya furaha kwamba atakuja baadaye. Na alisali ili Bwana atuwezeshe
kuelewa mambo haya .