2014-05-29 13:47:34

Jengeni urafiki wa dhati na Yesu Kristo!


Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kumwimbia Mwenyezi Mungu utenzi wa sifa na shukrani kwa kuhitimisha hija ya kitume iliyomwezesha kusherehekea Jubilee ya Miaka 50 tangu Papa Paulo VI alipokutana na kusali na Patriaki Anathegoras; kuwaimarisha wote wanaojibidisha katika mchakato wa kutafuta amani huko Mashariki ya Kati pamoja na kuwaimarisha ndugu zake katika imani.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anawaalika kujenga urafiki wa dhati na Yesu Kristo, ili waweze kumfuasa kwa ukaribu zaidi na hatimaye, kuishi pamoja na kwa ajili yake!







All the contents on this site are copyrighted ©.