2014-05-28 09:47:26

Wasichana waliotekwa nyara Nigeria waonekana walipofichwa!


Jeshi la Nigeria katika taarifa yake kwa vyombo vya habari linasema kwamba, limebaini mahali ambapo wasichana wa shule zaidi ya mia mbili waliotekwa nyara na kikundi cha Boko Haram mahali walipofichwa na kwamba, kwa sasa Jeshi halina mpango wa kutumia nguvu ili kuwaokoa wasichana hao ambao wanaendelea kunyanyasika chini ya udhalimu wa kikundi cha Boko Haram.

Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria amewatia shime askari wake ili kuendeleza mapambano dhidi ya kikundi cha Boko Haram kinachoendelea kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao! Serikali ya Nigeria haitaridhia masharti yaliyotolewa na Boko Haram ili kuwaachilia wasichana waliotekwa nyara. Mashambulizi ya Boko Haram nchini Nigeria yameendelea kuongezeka siku hadi siku kiasi cha kuhatarisha usalama na amani ya watu wengi!







All the contents on this site are copyrighted ©.