2014-05-28 10:36:00

Nia ya sala za Papa kwa Mwezi Juni yalenga kipeo cha kazi


Baba Mtakatifu Francisko kwa mwezi ujao Juni, ataelekeza nia zake kuu za sala, ili kwamba wale wasiokuwa na kazi waweze kupata msaada kwa mahitaji yao ya lazima au kupata kazi wanazohitaji kwa ajili ya kuishi maisha yenye hadhi na kiutu.
Na nia kwa sala ya kitume , ni ili Ulaya iweze kugundua upya mizizi yake ya Kikristu kupitia shuhuda za waamini. Emer McCarthy wa Radio Vatican, anaripoti kwamba, nia zote mbili , zinasisitiza utambuzi wa Papa juu ya hujuma za kiuchumi, zinazokumba bara la zamani la Ulaya, ambako mfumko wa gharama za maisha na ongezeko kubwa la ukosefu wa ajira, ni hoja kubwa katika majadiliano ya Baraza la EU na hasa wakati huu wa uchaguzi wa Madiwani.

Papa Francisko akijibu moja ya maswali aliyoulizwa Jumatatu jioni , akiwa ndani ya ndege kurejea Roma, juu ya matokeo ya uchaguzi nchini Italia , alikiri kujua kidogo juu ya mfumo wa serikali / siasa inayojali maoni na fikira za umma, barani Ulaya . Lakini aliasa matokeo ya ukosefu wa ajira katika jamii, ikiwa na maana ya ukosefu wa fedha haipaswi kupuuzwa. Alisema katika jamii kama hii ukosefu wa fedha na ajira hushamiri matendo maovu kama ya kutupa watoto , kuwapuuza wazee na vijana kubaki wakirandaranda ovyo bila tija... Na hili pia linajionyesha katika kuwa na kiwango kidogo cha uzazi, na ukumbatiaji wa mfumo wa euthanasia na vijana kukosa ajira, kiwango kilichofikia asilimia 40 %, nchini Italia, na asilimia 50% Hispania.

Papa Francis alionyesha kujali kwamba, kuna kizazi kizima cha watu ambao hawako masomoni wala kuwa na kazi. Utamaduni huu ni mbaya na Ulaya si peke yake inayoteswa na miundo mibovu ya mifumo ya kiuchumi ...
Papa alisistiza kwamba “ni muhimu kusisitiza tena kwamba, ajira ni muhimu kwa ajili ya jamii, kwa ajili ya familia na kwa ajili ya watu. Kazi ni tunu msingi katika ufanikishaji mazuri yote ya binadamu, kwa kuwa humfanya mtu binafsi ajisikie kuwa kamili kiakilia na kimatendo, hizia zake, ubunifu, mwelekeo na uwezo wake . Na hivyo, inaonekana kwamba, kazi si tu hulenga katika kupata faida za uchumi , lakini ni juu ya mambo yote kwamba, ni hadhi ya mtu mwenyewe. Na kama hakuna kazi , heshima hii hujeruhiwa! Hakika , wote wenye ajira na wasio ajiriwa huingia katika hatari ya kushushwa ngazi na kuwekwa pembezoni mwa jamii . Uwepo wa athari ya ubaguzi wa kijamii ".

Papa aliendelea kusema , Changamoto hii kubwa , na inahitaji ushiriki wa jumuiya ya Kikristo zima. Changamoto ya kwanza, ikiwa kufufua mizizi ya imani ya majitoleo kwa Yesu Kristo . Na huu ni msukumo msingi wa uchaguzi wa Kikristo: kuwa na imani . Imani ina uwezo wa kuhamisha milima! Imani ya Kikristo ina uwezo wa kuiimarisha jamii kupitia msingi na uhalisi wake wa maisha ya upendo na udugu wenye kuwajumuisha wote kwa pamoja ...na kamwe mwenye imani hapotezi matumaini kwa maisha bora ya baadaye! Kama kila mtu atafanya upande wake, kama sisi wote tutaheshimu ubinadamu na hadhi yake, na kama wote tutaimarisha tabia ya mshikamano na kugawana kidugu , kwa kuongozwa na Injili , tunaweza kuibuka kutoka dimbwi hili la kipindi kigumu na uzito wa uchumi unaoitikisa dunia.








All the contents on this site are copyrighted ©.