Maeneo ya Nchi Takatifu- yawezekana kuishi kwa amani-Papa .
Jumapili baada ya Ibada ya Misa, mjini Bethlehemu , Baba Mtakatifu Francisko aliekea
Jerusalem , ambako alipokelewa na Rais wa Jamhuri ya Israel, Shimon Peres na Waziri
Mkuu , Benjamin Netanyahu , katika uwanja wa ndege wa Ben Gourion wa Tel Aviv Jerusalem.
Katika hotuba ya mapokezi , viongozi hao walionyesha hofu kubwa kwa vurugu
zinazoendelea Mashariki ya Kati, ambako mara nyingi Wakristo huteswa. Na kwamba yawezekana
kuishi kwa amani katika eneo hilo lenye urithi mkubwa wa historia ya dini kuu tatu.
Wayahudi, Wakristu na Waislamu . Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu , katika hotuba
yake ya kumkaribisha Papa aliitaja, Israel kwamba imekuwa “kisiwa” cha uvumilivu
katika kuhakikisha haki kwa wote. Na kwamba wanapania kutetea haki za watu wote,
wanaoishi Maeneo Mtakatifu, licha ya tofauti za imani zao.
Na Papa Francisko
, katika hotuba yake , alitoa shukurani zake kwa moyo wa ukarimu na mapokezi mazuri
waliyompatia mara baada ya kuingia nchini Israel. Na kwamba kwake ilikuwa ni furaha
kuu kufanya hija katika nchi Takatifu akifuata nyayo za watangulizi wake, ambayo ina
historia ya miaka 50 iliyopita, iliyofanywa na na Papa Paulo V1.
Papa alikiri
tangu wakati ule hadi sasa , kuna mabadiliko mengi yaliyofanyika kati ya Jimbo Takatifu
na Nchi ya Israel, katika mahusiano ya Kidiplomasia , ambayo kwa sasa yanafikisha
miaka ishirini ya uwepo wake. Mahusiano yanayo endelea kufanikisha mwendelezo wa mahusiano
mazuri na urafiki , kama ilivyoshuhudiwa katika uwekaji wa sahihi katika makubaliano
na mikataba na njia ya kutembea pamoja katika kufanya marekebisho ya hapa na pale.
Kwa roho hiyo ya mshikamano na umoja Papa alitoa salaam zake za kipapa kwa watu wote
wa Israel na kuwatakia kila la heri, amani na ustawi wa kiroho na kihali pia. Hotuba
ya Papa, ilikumbusha msisitizo uliokwisha tolewa na watangulizi wake, katika kudumisha
historia na misingi ya urithi wa kuzaliwa kwa dini kuu tatu katika eneo hilo, Wayahudi,
Wakristu na Waislamu. Dini ambazo zote, msingi wake wa imani kiroho , umesimiskwa
katika kujali ubinadamu. Na hivyo Papa Fransiciko alionyesha tumaini lake kwamba katika
nchi hii Takatifu , hapatakuwa na nafasi , kwa wale wanao taka kutumia dini kama chombo
cha kuchochea kutovumiliana , ghasia na maonevu kwa yoyote yule. Papa aliendelea
kutaja kama hitaji la dharura, kufanikisha amani si tu kwa Israel lakini katika mkoa
wote wa Nchi Takatifu. Papa aliasa dhidi ya ongezeko la ghasia na uchokozi unaofanyika
mara kwa mara na kuvuruga imani na kusababisha mateso makubwa kwa watu .
Akiwa
ameshimana katika umoja na watu wote wenye mapenzi mema, Papa aliwataka wote wale
wenye kuwa na mamlaka , kuwajibika kikamilifu katika juhudi za upatikanaji wa majawabu
thabiti, ikiwemo ufutaji matatizo mazito yaliyopo kati ya Israel na Palestina , ili
wote waweze kuishi kwa amani na mapatano. Kwa upande wa Kanisa, kati ya walifika
kumlaki Papa katika uwanja huu wa Tel Aviv, ni pamoja na Nunsio wa Mjumbe wa Kitume
wa Papa nchini Israel, Askofu Mkuu Giuseppe Lazzarotto.