Azimio la Pamoja la Papa Francisko na Patriaki Bartholomeo I
Baba Mtakatifu Jumapili akiendelea na ziara yake, pia alikutana katika hali ya faragha
na Patriaki Barthlomew I, wa Kiekumene wa Costantinople , ukiwepo pia ujumbe wa
kitume wa Jerusalem na Katibu wa Vatican , Kardinali Pietro Parolin, na Mkuu a Shirika
kwa ajili ya Umoja wa Wakristu, Kardinali Kurt Koch Baada ya mkutano wao, kulitolewa
azimio la pamoja, la Papa Francisko na Partriaki Bartholomew 1, ambamo wametoa
heshima zao kwa watangulizi wao , Papa Paul VI na Patriaki wa Kiekumeni Athenagoras
, ambao walikuwa na ujasiri wa kukutana Yerusalemu miaka hamsini iliyopita. Na hivyo
wao pia , Papa Francisko na Patriaki Bartholomayo I , wamefanya mkutano wao katika
eneo hili la Nchi Takatifu, "ambapo mkombozi wetu Kristo Bwana, aliishi, kufundisha,
alikufa , akafufuka na akapaa mbinguni , ambapo yeye alimtuma Roho Mtakatifu juu ya
changa Kanisa kama pia maelezo yalivyo tolewa Papa Paulo VI na Patriaki Athenagoras
, yaliyo chapishwa baada ya mkutano wao , Januari 6, 1964.
Na pia wametaja
Mkutano wao wa ziada wa Maaskofu mjini Roma na Constantinople , katika mtiririko
wa udugu wa mitume wawili, Petro na Andrea, chanzo cha furaha na uthabiti wa kiroho,
wenye kuwapa nafasi ya kutafakari kina na uhalisi wa uhusiano kati yao , na matokeo
ya safari ndefu ya kuwa wamoja, iliyojaa neema hiyo ambayo Bwana, aliimimina kwao,
tangu siku hiyo heri ya miaka hamsini iliyopita .
Azimio limeendelea kutaja
kukutana kwao kindugu , kuwa ni hatua nyingine mpya na muhimu katika njia ya kuelekea
umoja ambayo Roho Mtakatifu pekee ndiye anaweza kuwaongoza katika ushirika wenye
kuwa na utofauti halali. Tunakumbuka kwa shukrani hatua ambazo Bwana tayari ametupa
kukamilisha.
3. Na kwa kufahamu kwamba, umoja huu, wazi ni upendo wa Mungu
na upendo kwa jirani , wao kwa muda mrefu, siku hadi siku, hatimaye wameweza kushiriki
pamoja katika karamu ya Ekaristi. Na kama Wakristo, wana wajibu wa kujiandaa kupokea
zawadi hii ya Ushirika Mtakatifu , kama alivyofundisha Mtakatifu Irenaeus wa Lyons
, kwa njia ya ungamo la imani na sala za pamoja za mara kwa mara,na kubadilika muono
wa ndani, upya wa maisha na mazungumzo ya kidugu (taz. Yn 13:35).
4. Kwa maana
hii, majadiliano muhimu kwa ajili ya kutafuta ushirika kamili kati ya Wakatoliki
na Wa-Orthodosi, yataendelea kama ilivyo katika majadiliano ya kitheolojia yanayo
fanywa na Tume ya Kimataifa ya Pamoja .
5.Wakiwa bado katika njia ya kuelekea
ushirika kamili , wao wana wajibu wa kutoa ushahidi katika kila hali za kawaida,
kuonesha upendo wa Mungu kwa ajili ya wote na kufanya kazi pamoja kwa ajili ya huduma
kwa ubinadamu , hasa kuhusiana na ulinzi wa hadhi ya binadamu katika kila hatua ya
maisha na heshima ya familia ya msingi juu ya ndoa , kukuza amani na manufaa ya wote,
kama jibu kwa taabu na mahangaiko yanayoendelea kuwa mapigo katika dunia yetu. Tunatambua
kwamba ni lazima daima, kuwa mstari wa mbele kusaidia watu wahitaji zaidi hasa wanaokabiliwa
na njaa, umaskini , ujinga, na usambazaji usiokuwa wa usawa wa bidhaa. Ni wajibu wetu
kujitahidi pamoja ili kujenga tu na ubinadamu jamii ambayo hakuna mtu kutengwa au
kubaguliwa.
6.Na kwa undani wanaamini kwamba, hali ya baadaye ya familia ya
binadamu inategemea sana kizazi cha sasa, na wao kama viongozi. Na hivyo baada ya
kupima kwa busara na upendo, na haki na usawa , na zawadi ya uongozi waliokabidhiwa
na Mungu na kisha kutubu, kutambua ugandamizaji haki unaoendelea duniani sasa,
, ambayo ni dhambi mbele ya Mungu, vinawathibitishia wajibu wao katika kulea hisia
ya unyenyekevu na kiasi , ili wote wapate hisi ya haja ya kuheshimu viumbe na kulinda
mazingira kwa uangalifu. Na hivyo kwa Pamoja , wamethibitisha wajibu wao wa kuamsha
dhamiri kuelekea ulinzi wa uumbaji , kwa kutoa Tunatoa wito, kwa wanaume na wanawake
wote wenye mapenzi mema kuangalia, njia yao ya maisha, kwa moyo wa kiasi zaidi ,na
kuzimisha moyo wa uchoyo na kuinua zaidi ukarimu, kwa ajili ya ulinzi wa ulimwengu
wa Mungu na kwa manufaa ya watu wake.
7. Pia kuna haja ya haraka kwa ajili
ya ushirikiano thabiti na kutimiza ahadi miongoni mwa Wakristo, ili kulinda kila
mahali haki ya kutoa hadharani imani yao na kutendewa haki wanapo timiza nia ya
kukuza mchango kwamba Ukristo ni sehemu ya maisha kwa jamii na hata katika utamaduni
wa kisasa . Katika suala hili , tunawaomba Wakristo wote kukuza mjadala wa kweli na
Wayahudi, na Uislamu na mila nyingine za kidini. Kutofautiana na utoaji wa majibu
bila ufahamu, huweza tu kusababisha kukosa uaminifu na kwa bahati mbaya, hata migogoro.
8.
Kutokana na hili, wakiwa katika Mji Mtakatifu wa Yerusalemu , walipenda kueleza
wasiwasi wao, kwa hali ya kawaida ya Wakristo katika Mashariki ya Kati na kwa haki
yao ya kuwa raia kamili ya nchi zao .Na kwa ujasiri walitolewa maombi yao kwa Mwenyezi
Mungu mwenye huruma kwa ajili ya amani katika Nchi Takatifu na Mashariki ya Kati
. Wanaomba hasa kwa ajili ya makanisa nchini Misri , Syria na Iraq, ambako yanakumbana
na mateso makali, kama iliyokuwa katika matukio ya hivi karibuni . Na hivyo wanahimiza
pande zote , bila kujali imani za dini zao , kuendelea kufanya kazi kwa maridhiano
na kwa kutambua haki sahihi za watu . Kwa undani wanaamini kwamba silaha si nyenzo
ya kujenga amani ya kudumu, bali njia mazungumzo , msamaha na upatanisho ndiyo njia
sahihi ya kuifikia amani ya kweli.
Na hivyo wametoa wito kwa Wakristo, waamini
wa mila zote za kidini na watu wote wenye mapenzi mema , kutambua kama jambo la dharura
, kuushiriki kikamilifu juhudi zote zinazo tafuta maridhiano na umoja wa familia
ya kibinadamu , kwa heshima kamili kwa ajili ya tofauti halali kwa ajili ya mema ya
binadamu wote na kwa vizazi vijavyo.
Na wakiwa katika Hija hii ya kawaida na
mahali ambapo Bwana wetu pekee, Yesu Kristo alisulubiwa , akazikwa na kufufuka tena
, kwa unyenyekevu, wanajikabidhi katika maombezi ya Mama Bikira Maria, katika kupata
ujasiri wa kutembea pamoja katika safari hii ya kuelekea umoja kamili, katika Upendo
wa Mungu usiokuwa na mwisho kwa ajili ya familia nzima ya binadamu.
"Bwana
na akuangazie uso wake na huruma yake . . Bwana akuonyeshe uso wake na kukupa amani
"( Nm 6, 25-26).