Rais Jacob Zuma aliyeshinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni nchini
Afrika ya Kusini, Jumamosi tarehe 24 Mei 2014 ameapishwa rasmi na kuanza kuwaongoza
wananchi wa Afrika ya Kusini katika awamu ya pili ya uongozi wa Serikali yake.
Tukio
hili limeandamwa na maandamano ya kumpinga Rais Zuma kwamba ni kiongozi ambaye hastahili
kuwaongoza wananchi wa Afrika ya Kusini kutokana na kashfa ya ufisadi wa mali ya umma
inayomwandama, kwa kutumia kiasi cha dolla za kimarekani millioni 23 kwa ajili ya
ukarabati wa nyumba yake binafsi.
Rais Zuma anashutumiwa pia kwa kuitumbukiza
Afrika ya Kusini katika hali mbaya ya uchumi. Pamoja na mambo yote haya wachunguzi
wa mambo wanasema, demokrasia imeshika mkondo wake na wananchi wa Afrika ya Kusini
wamemchagua Rais Zuma kuwaongoza tena kwa awamu ya pili! Tukio hili limehudhuriwa
na viongozi mbali mbali kutoka Afrika!