2014-05-24 12:03:48

Roho Mtakatifu ni kocha wa maisha ya kiroho!


Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican inapenda kukushirikisha utajiri wa tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya Vi ya Kipindi cha Pasaka inayomwonesha Roho Mtakatifu kuwa kweli ni kocha na mwalimu wa maisha ya kiroho! Kazi kwako!

Katika Injili NENO KUPENDA/PENDO linatawala – hivi unajisikiaje unapoambiwa nakupenda au unapohisi kuwa unapendwa? Hakika kupenda kunawajibisha - tamko hilo lasubiri jibu. Wengi wetu twafahamu fika jinsi ilivyo vigumu kupenda upeo/kweli. Upendo unadai matendo. Kinachofuata ni wajibu.


Ndicho kinachoonekana katika masomo yetu ya leo = kutii amri na kuabudu. Ndiyo maana Yesu anaweza kusema mkinipenda mtazishika amri zangu. Mtakatifu Tomas wa Akwino - sheria za Mungu ni nyepesi kwa wapendao na mzigo kwa wasiopenda.

1 Jan 4,8 yeye asiyependa hakumjua Mungu kwa maana Mungu ni upendo -hivyo ili kupenda vizuri ni lazima kumjua Mungu sababu yeye ni PENDO. Mapendo ya kweli yadai sadaka. Ili kushika amri au sheria inavyotakiwa yahitaji sadaka kubwa na inayodai utumishi.

Mt Agustino anapotafakari juu ya upendo wa Mungu anasema - umegusa mioyo yetu kwa pinde za upendo wako na akili zetu kwa mishale ya neno lako.

Baada ya utangulizi na kusikia masomo kinachotakiwa na kuweka katika matendo. Ndicho kinachoonekana katika masomo yetu na baada ya kuelewa kuishi.

Katika somo la 1 - Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani ya Petro. Ubatizo wetu unatuwajibisha. Sisi tumebatizwa kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Tumezamishwa ndani yake Mungu, katika Utatu Mtakatifu. Sisi tunashiriki ile asili ya Kimungu. Hatuitwi kwa jina linguine ila ni watoto wa Mungu na ndivyo tulivyo.

Katika somo la 2 - Twaona wingi wa neema ya tendo la Mungu la kuokoa na hitaji la utayari wa mkristo. Petro anasema mpokeeni Kristo, na ondoeni roho ya woga. Halafu Petro asema - kuweni na uwezo wa kuelezea imani yenu - ni kwa ajili yake twafanya mambo haya. Imani yetu na maisha yetu - msingi wake ni Kristo aliyekufa na akafufuka. Sababu ya matumaini yetu – inaonekana katika ukuaji wa ufalme wa Mungu na kumpenda Mungu. Matumaini yetu ni ufalme wa Mungu, utukufu wa Mungu, upendo wake, ujio wa mbingu mpya na nchi mpya, ujio wa ufalme wa haki na amani. Tukumbuke kuwa Roho wa Mungu hushuhudiwa na anatakiwa aonekane katika maisha yetu ya kila siku. Gal. 5:22-23 – lakini matokeo ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, hisani, ukarimu, uaminifu, upole na kiasi.

Katika Injili - Baba atampa Roho Mtakatifu

Hivyo tunamwona Baba anayependa kwa njia ya Roho Mtakatifu na Mwanaye.

Hivyo Petro na Yohani wanaondoka kwenda kutangaza habari njema na wale waliobatizwa na Filipi wakawekewa mikono na kupokea Roho Mtakatifu. Na hapo yaonekana mwanzo wa mitume kwenda kuhubiri habari njema duniani.

Ndiyo maana sisi tumeitwa kuitikia huu mwito – kuishi kadiri ya amri za Mungu. Mambo haya mawili hayatengani - upendo na utii.

Hii ndiyo kazi kuu ya Roho Mtakatifu - Huyu Roho anayepelekwa atawezesha udumifu wetu katika maisha ya ukristo.

Huyo Roho = wakili, mfariji, mshauri msaidizi.

Kigiriki ni yule anayesimama kando ya mteja na kwa lugha ya kisheria ni mwanasheria, wakili. Pengine lugha ya siku hizi ni tungesema ni kocha, mwalimu. Roho Mtakatifu yupo nasi pamoja na anatuongoza, sahihisha.

Twaweza kujiuliza kwanini twahitaji huyu roho mtakatifu? Majibu yako mengi;


Peke yetu bila Mungu hatuwezi kitu. Watu wengi huamini na kudhani kuwa hawana haja ya msaada, ushauri, mawaidha kushirikiana na wengine n.k. Je ni kweli.

Katika mojawapo ya mafundisho ya Papa Benedict XVI kabla ya uteuzi – akiongea dhidi ya watu wanaoishi bila mwelekeo - wanaodhani kuwa hawahitaji Mungu wa mwanadamu mwenzio – anasema matokeo yake huwa kinyume cha wote.

Ni kwa jinsi gani tunaweza kupokea hiyo zawadi ya Mungu? Huyo Roho Mtakatifu?

Ni katika kuishi amri ya mapendo kwa Mungu na jirani Yoh 14,15-16

Baada ya kupaa Bwana mitume na wanawake walienda chumba cha juu – wakisali na kusubiri - Mdo 1,14 hatuna budi nasi kufanya hivyo. Kipindi kati ya kupaa Bwana na Pentekoste ni kipindi cha sala na subira - tukijiandaa kumpokea Roho mtakatifu. Sote tunaalikwa kufanya hivyo - tunamhitaji mwalimu, kiongozi n.k - leo kama iliyokuwa miaka 2000 iliyopita.

Mungu ametupa pendo na amri - sisi tumetoa nini?

Na Padre Reginald Mrosso, C.PP.S.
Dodoma.








All the contents on this site are copyrighted ©.