2014-05-22 08:27:59

Monsinyo Fabio Fabene kuwekwa wakfu 30 Mei 2014


Baba Mtakatifu Francisko tarehe 30 Mei 2014 majira ya jioni anatarajiwa kumweka wakfu Monsinyo Fabio Fabene, Katibu mkuu msaidizi wa Sinodi za Maaskofu kuwa Askofu, ili kuimarisha mchakato wa utekelezaji wa maadhimisho ya Sinodi kama chombo muhimu sana katika maisha na utume wa Kanisa.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Fabio Fabene alizaliwa mjini Roma, tarehe 12 Machi 1959. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa tarehe 26 Mei 1984. Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu hapo tarehe 8 Aprili 2014.







All the contents on this site are copyrighted ©.