2014-05-22 12:11:14

Makardinali wapangiwa Mabaraza ya Kipapa


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 22 Mei 2014 amewapangia Makardinali wapya waliosimikwa kwenye Ibada iliyofanyika hapo tarehe 22 Februari 2014 Mabaraza ya Kipapa watakayoshiriki kama wajumbe. Kutoka Barani Afrika Makardinali wamepangiwa Mabaraza ya Kipapa yafuatayo:

1. Kardinali Philippe Nakellentuba Ouèdraogo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Ouagadougou atakuwa mjumbe wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu pamoja na Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini.

2. Kardinali Jean -Pierre Kutwa, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Abijan, Pwani ya Pembe atakuwa mjumbe wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za kitume. Ameteuliwa pia kuwa mjumbe wa Baraza la Kipapa la Walei pamoja na Baraza la Kipapa la Haki na Amani.









All the contents on this site are copyrighted ©.