2014-05-21 09:02:26

Viongozi, msilee misimamo mikali ya kidini!


Misimamo mikali ya kidini ni kati ya changamoto kubwa zinazotishia amani, utulivu na usalama katika nchi nyingi Barani Afrika. Vita na kinzani za kijami zinazoendelea kujitokeza sehemu mbali mbali Barani Afrika zina chanzo chake katika misimamo mikali ya kidini, hali ambayo imepekea hata kuwepo pia kwa mashambulizi ya kidaidi.

Kumbe, kuna haja kwa Serikali na viongozi wa dini Barani Afrika kushirikiana kwa pamoja ili kuondokana na tatizo la watu wenye misimamo mikali ya kiimani ambao wanaendelea kuwa ni tishio katika kudumisha misingi ya haki, amani na utulivu. Ni changamoto iliyotolewa na Rais Ismail Omar Guelleh wa Gjibout alipokuwa anazungumza na wakuu wa dini ya Kiislam kutoka Gjibout, Ethiopia, Sudan, Somalia, Yemen na Saud Arabia waliokuwa wanajadili tatizo la misimamo mikali ya kidini Afrika Mashariki.

Baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislam wanasema, leo hii kutokana na vitendo vya mashambulizi ya kigaidi kutokana na misimamo mikali ya kiimani sanjari na vitendo vya kigaidi, kuna tafsiri mbali mbali zinazotolewa pengine hata kinyume cha ukweli wa dini ya Kiislam, hali ambayo inachafua dini ya Kiislam katika ujumla wake kutokana na vitendo vya watu wachache ndani ya Jamii.







All the contents on this site are copyrighted ©.