2014-05-21 07:54:15

Majadiliano ya kidini ni muhimu katika ujenzi wa amani duniani!


Zaidi ya Marabbi 400 pamoja na watu mashuhuri kutoka Marekani wamemwandikia Baba Mtakatifu Francisko ujumbe wa matashi mema, huku wakimkaribisha kwa mikono miwili kutembelea Israeli wakati huu wa hija yake ya kichungaji inayoanza tarehe 24 hadi tarehe 26 Mei 2014 kwa kuongozwa na kauli mbiu "wote wawe wamoja".

Ujumbe huu unatarajiwa kuchapishwa kwenye magazeti mashuhuri nchini Israeli, Jumapili ijayo. Hizi ni harakati za kutaka kujenga na kudumisha majadiliano ya kidini kati ya Wayahudi na Wakristo, kwani viongozi hawa wanasema kwamba, majadiliano ya kidini ni muhimu sana katika mchakato wa watu kufahamiana na kuheshimiana na hatimaye, kujenga umoja, udugu na mshikamano.

Baba Mtakatifu Francisko anasema, lengo la maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro ni kutaka kujenga daraja la amani duniani!







All the contents on this site are copyrighted ©.