Wakulima wadogowadogo bado ni muhimu katika upatikanaji wa chakula
Zaidi ya watalaam 800 kutoka sehemu mbalimbali za dunia , walikusanyika pamoja mjini
Addis Ababa Ethiopia, kujadili changamoto na uwekezaji unaohitajika kufanikisha lengo
la kutokomeza utapiamlo na njaa duniani. Katika mkutano huo ilielezwa kwamba, wakulima
wadogowadogo bado ni nguzo ya uzalishaji wa chakula duniani, kwa utambuzi kwamba,
zaidi ya watu milioni 500 ni wakulima wa mashamba madogomadogo ya kifamilia, ambayo
huzalisha hadi asilimia 80 ya chakula kinacho tumiwa na nchi zenye viwanda vichache. Dk
Kanayo F. Nwaze , Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo ( IFAD)wakati
akishiriki katika mkutano huo wa Kimataifa juu ya Sera za Chakula na Tafiti( IFPRI)
2020, alisisitiza kuwekeza katika mifumo jasiri ya wakulima wadogo wadogo, ambayo
imekuwa kwa miaka mingi njia kuu upatikanaji wa chakula cha jamii na uwiano endelevu
katika maendeleo ya mataifa."
Kwa mujibu wa IFPRI, ajenda baada ya malengo
ya 2015, inapaswa kufuta njaa ifikapo mwaka 2025, lakini hii inaweza tu kufanikiwa
" kwa kujenga ujasiri wa mazingira , kisiasa na kiuchumi na kuondokana na majanga
mbalimbali yanayo tishia usalama wa chakula na maisha .
Mkuu wa IFAD, alionyesha
imani yake kwenye umuhimu wa kujenga ujasiri kwa wakulima wadogo wadogo , ambao bahati
mbaya, mara kwa mara hupambana na nyakati ngumu. Alisema , wao bila ya chaguzi, huwekeza
katika kilimo hata nyakati za migogoro, wakihatarisha msingi wa mali yao, bila ya
kuwa na bima,wala kuwa na dhamana katika huduma za fedha na mifumo ya usalama ya
kijamii. Matokeo yake ni kuchukua hatua kali kama vile kuondoa watoto kutoka shule,
kuuza kila kitu chao, kukusanyika na kuhamia mijini. Hivyo nchi zinapaswa kusaidia
wakulima wadogo wadogo katika kukuza umiliki na uhakika wa ustawi endelevu.
Ripoti
iliyotolewa katika kikao hicho iliwaangalisha washiriki wa mkutano kwamba, katika
kipindi cha miaka mitano peke yake, dunia imeshuhudia tetemeko kubwa la ardhi huko
Haiti ; ukame katika Pembe ya Afrika ; tetemeko la ardhi la tsunami ulio sababisha
mgogoro wa nyuklia Japan; na kupanda kwa bei za vyakula mwaka 2008 ambako bado kunaathiri
bei za vyakula duniani hata leo . Aidha katika kipindi cha miezi sita peke yake iliyopita,
Kimbunga Haiyan kilicho tokea Ufilipino, mafuriko makubwa yaliyopiga Uingereza; vita
vya wenyewe kwa wenyewe imeendelea katika Jamhuri ya Afrika ya Kati , Syria, na Sudan
ya Kusini; maporomoko ya ardhi yaliyo vuruga Afghanistan; na ugonjwa mpya iitwayo
katika nji aya pumua hewa mwilini uliojitokeza katika Peninsula ya Arabia, ni maafa
yasiyoweza kusahaulika. Nayo Ripoti ya hivi karibuni kutoka Jopo la Kimataifa ya Hali
ya Hewa Change ( IPCC) pia alithibitisha jukumu binadamu katika kusababisha mabadiliko
ya hali ya hewa na imeonya kutokea kwa majanga zaidi.
Na Mkurugenzi Mkuu wa
IFPRI, Sheggen Fan, alisema, kuna uwezekano wa majanga mengi kuzuiwa katika uso wa
dunia, iwapo binadamu wote watapania kwa nia moja kujenga mafanikio licha ya kukabiliana
majanga. Na hilo litategemea jitihada mpya katika kushirikamana na umoja katika
ajenda ya ujasiri.
Aidha ameeleza juhudi za Umoja wa Mataifa kusaidia familia
kukabiliana na nyakati ngumu kwa njia endelevu, hufanyika pia kupitia Mpango wa Chakula
WFP) ambao hufanya kazi kwa mujibu jadi yake ya kutoa msaada wa chakula, kuchangia
asilimia 40 ya shughuli zake na mipango inayo andaliwa na kuhamasisha ujasiri. Dk
Ertharin Cousin , Mkurugenzi Mtendaji wa EFP, Pa alielezea imani yake kwamba mchakato
wa kufikia ujasiri lazima kuanza na dhana ya kuhama katika kufikiri. " Ujasiri inahitaji
uelewa wa maisha ya jamii , " alisema.
Na ni muhimu kuwa na mageuzi ya matazamio
na mawazo mapana zaidi umiliki wa mali za kudumu zaidi ya umiliki wa nyumba, na
kuingia katika ubia wa sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa kila mwanamme
na mwanamke anawezeshwa kuchagia kwa kiwango kikubwa uwezo wake katika maamuzi na
utendaji. Na kwamba mahitaji ya dunia yanahitaji kupitishwa kwa ujasiri kutoa gawio
linganifu, hata kwa jamii tete ambazo leo hii katika uso kimazingira, kiuchumi, na
lishe zinaonekana kufilisika. "
Aliongeza kuwa, jumuiya zilizoathirika na ukame,
mafuriko , na majanga mengine, mbinu ya ujasiri inaruhusu uchukuaji wa hatua za kina
kurudisha maeneo ya kuishi na uzalishaji kwa lengo la kboresha ustawi wao. Ajenda
zenye kuimarisha ujasiri zitawezesha familia kuwa imara na kuhimili mshtuko, na hivyo
kurudi katika juhudi za uazalishaji hasa chakula kwa ajili yao na watoto wao.