2014-05-16 08:26:56

Nigeria sasa kula sahani moja na Boko Haram hadi kieleweke!


Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria baada ya kupata shinikizo kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa amefafanua kwamba, hakuna uwezekano wa kubadilishana wafungwa wa Kikundi cha kigaidi cha Boko Haram na wanafunzi waliotekwa nyara hivi karibuni Kaskazini mwa Nigeria.

Rais amefafanua hayo wakati alipokutana na kuzungumza na Bwana Mark Simmonds afisa wa Deski la Afrika kutoka Uingereza, ambaye yuko nchini Nigeria ili kubainisha mchango wa Uingereza katika mapambano dhidi ya Kikundi cha kigaidi cha Boko Haram. Amekazia kwamba, hakutakuwa na mjadala na magaidi, hadi kieleweke!

Jumamosi, tarehe 17 Mei 2014, Ufaransa imeandaa mkutano wa kimataifa unaotarajiwa kuzungumzia kuhusu vitisho vya Boko Haram na unatarajiwa kuhudhuriwa na Marais kutoka Benin, Cameroon, Chad na Niger!







All the contents on this site are copyrighted ©.