Gavana mkuu wa New Zealand akutana na Papa mjini Vatican
Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 15 Mei 2014 amekutana na kuzungumza na Gavana
mkuu wa New Zealand Bwana Jerry Mateparae ambaye baadaye amkutana na Kardinali Pietro
Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Dominique Mamberti,
Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.
Katika
mazungumzo yao, viongozi hawa wawili wamejikita zaidi katika maisha ya kijamii na
kiuchumi nchini New Zealand sanjari na mchango wa Kanisa Katoliki katika ustawi na
maendeleo ya wananchi katika medani mbali mbali za maisha. Wamebadilishana mawazo
kuhusiana na masuala ya kimataifa, lakini kwa namna ya pekee mchakato wa ushirikiano
wa kikanda katika mikakati ya maendeleo endelevu pamoja na ushiriki wa utunzaji wa
amani sehemu mbali mbali za dunia.