2014-05-11 09:44:35

UNICEF inaungana na wanawake wa Nigeria kwa Siku ya Mama Duniani 2014


Shirika la kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF katika taarifa yake kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Mama Duniani kwa Mwaka 2014 linapenda kuitolea kwa ajili ya akina mama wa Nigeria ambao wanaendelea kuwalilia watoto wao waliotekwa nyara na Kikundi cha Boko Haram huko Nigeria. Ni matumaini ya UNICEF kwamba, wasichana hawa wataweza kuachiliwa mara moja, ili kujiunga na familia zao pamoja na kuendelea na masomo.

UNICEF inasema katika taarifa yake kwamba, hali ya afya ya Mama na Mwana inendelea kuboreka sehemu mbali mbali duniani na kwamba, vifo vya akina mama wajawazito na watoto kwa mwaka 2013 vimepungua kwa asilimia 45% ikilinganishwa na hali ilivyokuwa katika miaka ya 1990. Wanawake 289, 000 walifariki dunia kutokana na matatizo ya kujifungua, ikilinganishwa na wanawake 523, 000 waliofariki dunia katika kipindi cha mwaka 1990. Maboresho ya afya ya mama na mwana ni matokeo ya kampeni ya chanjo zinazotolewa.







All the contents on this site are copyrighted ©.