2014-05-11 09:58:31

ANC yaibuka kidedea uchaguzi mkuu Afrika ya Kusini


Tume ya uchaguzi nchini Afrika ya Kusini imekamilisha zoezi la kuhesababu kura na kutangaza kwamba, Chama tawala cha ANC kimeshinda kwa asilimia 62.2% na kwamba, Chama cha upinzani cha Democratic Alliance kimepata asilimia 22.23% ya kura zote zilizopigwa, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 5%, ikilinganishwa na kura za mwaka 2009. Chama cha Economic Freedom kinachotaka kuwagawia maskini utajiri wa nchi kimepata asilimia 6.35%.

Taarifa inaonesha kwamba, wananchi wa Afrika ya Kusini waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi mkuu uliomalizika walikuwa ni sawa na asilimia 73% ya wananchi millioni 25 wa Afrika ya Kusini. Hii ni sawa na asilimia 50% ya idadi ya wananchi wote waliojiandikisha kupiga kura. Rais Jacob Zuma anasema anapania kuboresha huduma msingi za kijamii kwa wananchi wengi wa Afrika ya Kusini.







All the contents on this site are copyrighted ©.