2014-05-10 10:52:25

RENAMO kushiriki uchaguzi mkuu nchini Msumbiji


Bwana Alfonso Dhlakama Mwenyekiti wa Chama cha Upinzani cha RENAMO nchini Msumbiji ni kati ya viongozi waliojiandikisha katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba, 2014 nchini Msumbiji. Kwa kutangaza nia ya kushiriki katika uchaguzi mkuu, Bwana Alfonso Dhlakama ametoka rasmi mafichoni ambako alikuwa amejificha baada ya hali ya kisiasa nchini Msumbiji kuanza kuchafuka tena kwa RENAMO kutishia kurudi tena msituni ili kuendesha vita.

RENAMO imetangaza kusitisha mashambulizi katikati ya Msumbiji, ambako kwa miaka miwili, RENAMO kimekuwa kikipambana na Jeshi la Serikali ya Msumbiji. Eneo linalohusika kadiri ya taarifa ya vyombo vya habari ni katika Jimbo la Sofala, Msumbiji.







All the contents on this site are copyrighted ©.