2014-05-09 07:35:28

Shukrani na pongezi kwa Jeshi la Polisi Italia kwa kuadhimisha Miaka 162 tangu akuanzishwa!


Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Italia, Kamanda Alesandro Pinsa anapenda kulishukuru kwa dhati Jeshi la Polisi Italia kwa huduma ya ulinzi na usalama linalotoa kwa wananchi, kwa takribani miaka 162 tangu lilipoanzishwa.

Baba Mtakatifu anatambua fika mchango unaotolewa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mji wa Vatican katika kusimamia matukio mbali mbali yanayohusu maisha na utume wa Kanisa.







All the contents on this site are copyrighted ©.