2014-05-07 08:07:03

Papa atembelea ofisi za Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne asubuhi tarehe 6 Mei 2014, akiwa ameambatana na Askofu mkuu Angelo Becciu, katibu mkuu msaidizi wa Vatican alitembelea Ofisi za Sekretarieti ya Vatican, kukutana na kusalimiana na wafanyakazi katika ofisi hizi, kama sehemu ya mikakati yake ya kichungaji ya kufahamiana kwa karibu zaidi na wale wanaomsaidia kutekeleza utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Itakumbukwa kwamba, tarehe 15 Aprili 2014, Baba Mtakatifu alitembelea baadhi ya ofisi za Sekretarieti ya Vatican. Baba Mtakatifu anaendelea kuwashukuru wafanyakazi wote wa Vatican kwa sadaka, majitoleo na huduma yao kwa Kanisa la Kristo.







All the contents on this site are copyrighted ©.