2014-05-06 10:11:39

Nigeria inaomba msaada wa kimataifa dhidi ya Boko Haram!


Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria anaomba msaada kutoka katika Jumuiya ya Kimataifa ili kukabiliana na Kikundi cha Kigaidi cha Boko Haram ambacho kinaendelea kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Rais Jonathan anasema amekwisha omba msaada wa kiufundi kutoka: Marekani, Uingereza, Ufaransa na China.

Marekani imeonesha nia ya kusaidia juhudi za Serikali ya Nigeria ili kupambana na Kikundi cha Boko Haram, kwa kuimarisha miundo mbinu pamoja na Jeshi la Nigeria ili liweze kupambana zaidi na mashambulizi pamoja na uvunjifu wa haki msingi za binadamu.

Rais Jonathan amezungumza kuhusu mkakati wa Serikali katika mapambano dhidi ya Kikundi cha kigaidi cha Boko Haram ambacho kwa siku za hivi karibuni kiliteka wasichana wa shule Chibok, iliyoko Kaskazini Mashariki mwa Jimbo la Borno, ngome ya Boko Haram.







All the contents on this site are copyrighted ©.