2014-05-06 09:37:57

Mwezi wa Rozari Takatifu!


Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anatarajiwa tarehe 8 Mei 2014 kuongoza Ibada ya Rozari Takatifu, muhtasari wa Injili kwa maelfu ya waamini na watu wenye mapenzi mema watakaokuwa wamekusanyika kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa Pompei, Napoli, Kusini mwa Italia. Waamini watasali sala iliyotungwa na na Mwenyeheri Bartolo Longo kunako mwaka 1883.

Waamini kuanzia tarehe 6 Mei 2014 wameanza maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 75 tangu kutabarukiwa kwa Kanisa kuu la Pompei kwa maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu, mkesha na sala ya Rozari Takatifu. Kardinali Pietro Parolin anatarajiwa kuongoza Ibada ya Misa Takatifu Alhamisi, tarehe 8 Mei 2014 na baadaye sala ya Rozari takatifu majira ya mchana.

Ibada hii inatarajiwa kuhudhuriwa na Maaskofu kutoka Kusini mwa Italia, waamini pamoja na viongozi mbali mbali wa Serikali







All the contents on this site are copyrighted ©.