2014-05-05 12:22:55

Askofu Gervas Nyaisonga asimikwa rasmi Jimbo Katoliki Mpanda


Askofu mkuu Francisco Montecillo Padilla, Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Jumapili tarehe 4 Mei 2014 ameadhimisha Ibada ya kumsimika rasmi Askofu Gervas Nyaisonga kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Mpanda. Ibada hii imehudhuriwa na Maaskofu na viongozi mbali mbali kutoka ndani na nje ya Jimbo Katoliki Mpanda.

Katika mapokezi ya Askofu Nyaisonga Jimboni Mpanda, Padre Martini Kapufi (42) aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Mwese, Jimbo katoliki Mpanda na Katekista Patrick Mwendowasaa (60) walifariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka baada ya kuacha njia. Waliolazwa hospitalini kwa matibabu zaidi ni Katekista Daud Saveli na Melkior Malaluma, mwamini.







All the contents on this site are copyrighted ©.