2014-04-29 08:45:37

Mpasuko mkubwa ndani ya Chama cha MDC Zimbabwe!


Chama cha upinzani nchini Zimbabwe MDC kimepata mpasuko mkubwa baada ya aliyekuwa Waziri mkuu wa Zimbabwe Bwana Morgan Tsvangirai kuondolewa kwenye Chama kwa shutuma za kutaka kuwadhibiti wapinzani wake ndani ya chama kinyume cha kanuni na taratibu za kidemokrasia.

Kundi la upinzani linaundwa na Bwana Tendai Biti, aliyekuwa Waziri wa fedha katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini Zimbabwe. Wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanasema kwamba, Bwana Tsvangiraia akitaka kumdhibiti na hatimaye kummaliza kisiasa Bwana Tendai Biti.

Mpasuko huu mkubwa ambao hujawahi kutokea umeendelea kukidhohofisha chama cha MDC ambacho katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka uliopita kilishindwa kufua damu mbele ya Rais Robert Mugabe aliyeibuka kidedea!







All the contents on this site are copyrighted ©.