2014-04-28 14:10:47

Shukrani kwa Mwenyezi Mungu!


Kardinali Stanislaw Dziwisz, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Krakovia, Poland katika Ibada ya shukrani iliyofanyika kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican Jumatatu tarehe 28 Aprili 2014 anamshukuru Mungu kwa kumwezesha Mtakatifu Yohane Paulo II, Baba wa huruma ya Mungu, kutekeleza kwa dhati kabisa mafundisho ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican pamoja na kuliandaa Kanisa kuingia katika Millenia ya tatu ya Ukristo.

Kardinali Dziwisz anasema, shukrani hizi ni kutokana na ushuhuda angavu na wa kweli unaojikita katika upendo na huduma kwa wote, kama walivyoonesha watakatifu hawa wapya katika maisha na utume wao kama viongozi wakuu wa Kanisa. Waamini wanamshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa kuridhia ombi la kuwatangaza Mapapa hawa wawili kuwa Watakatifu, mchakato ambao ulianzishwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI, tukio muhimu sana kwa ajili ya Kanisa zima.







All the contents on this site are copyrighted ©.