2014-04-28 14:30:05

Mfalme Juan Carlos na Malkia Sofia wakutana na Papa Francisko mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 28 Aprili 2014 amekutana na kuzungumza na Mfalme Juan Carlos na Malkia Sofia ambao baadaye walikutana pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Dominique Mamberti, katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Katika mazungumzo hayo kati ya Baba Mtakatifu na wageni wake, wamegusia kuhusu uhusiano wa dhati uliopo kati ya Vatican na Hispania ambao umeendelea kuimarishwa tangu mwaka 1979 wakati nchi hizi mbili zilipotiliana sahihi mkataba wa ushirikiano. Wameangalia pia hali halisi na utume wa Kanisa nchini Hispania. Viongozi hawa wamebadilisha mawazo kuhusu mambo msingi ya kimataifa kwa kujikita zaidi katika kinzani na migogoro inayoendelea kufuka moshi sehemu mbali mbali za dunia.







All the contents on this site are copyrighted ©.