2014-04-27 12:01:42

Walioguswa na miujiza ya Mtakatifu Yohane Paulo II


Mama Floribeth Mora Diaz, aliyepata bahati na neema ya kupona kutokana na ugonjwa wake kwa maombezi ya Mtakatifu Yohane Paulo II, ndiye aliyeteuliwa kubeba Masalia ya Mtakatifu Yohane Paulo II wakati wa Ibada ya Misa Takatifu, kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vaticam siku ya Jumapili tarehe 27 Aprili 2014.

Masalia ya Mtakatifu Yohane XXIII yamebebwa na wapwa zake wanne, waliokuwa wameongozana na Meya wa Mji wa Sotto Il Monte, Mstahiki Eugenio Bolognini ambaye pia ni Rais wa Mfuko wa Yohane XXIII. Sr. Marie Simon-Pierre, aliyeponywa kutokana na maombezi ya Mtakatifu Yohane Paulo II amesoma ombi kwa lugha ya Kifaransa katika Ibada hii.All the contents on this site are copyrighted ©.