Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kuwatangaza Wenyeheri Yohane XXIII na Yohane Paulo
II kuwa watakatifu imehudhuriwa na umati mkubwa wa waamini na watu wenye mapenzi mema
kutoka sehemu mbali mbali za duni.
Marais kutoka Barani Afrika waliohudhuria
katika Ibada hii ni: Rais Paulo Biya kutoka Cameroon, Rais Ali Bongo Ondinba kutoka
Gabon na Rais Robert Mugabe kutoka Zimbabwe.
Taarifa rasmi inaonesha kwamba,
kulikuwa na ujumbe wa waamini kutoka katika dini mbali mbali. Kutoka Afrika kulikuwa
na ujumbe wa: Serikali ya Angola, Burkina Faso, Burundi, Cameroon Cape Verde, Pwani
ya Pembe, Gabon, Ghana, Guinea Bissau, Equitorial Guinea, Lesotho, Liberia, Msumbiji,
Namibia, Niger, Nigeria, DRC, Sudan, Tanzania, Togo, Uganda, na Zimbabwe.