2014-04-24 16:09:54

Tunataka Katiba itakayodumisha misingi ya haki, amani na mshikamano wa kitaifa!


Mama Helan Moshi kutoka Jimbo kuu la Dar es Salaam ni kati ya mahujaji kutoka sehemu mbali mbali waliofika mjini Roma ili kushuhudia Wenyeheri Yohane XXIII na Yohane Paulo II walitangazwa kuwa Watakatifu, Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. RealAudioMP3

Anasema, wakati huu anapofanya hija ya maisha ya kiroho ili kumshukuru Mungu kwa kuliwezesha Kanisa kupata miamba haw wa imani, sala na mawazo yake bado anayaelekeza Tanzania, akiwaomba Wenyeheri hawa kuiombea Tanzania ili iweze kuwa na amani, upendo na mshikamano wa kitaifa.

Anawasihi sana wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutambua kwamba, wameteuliwa ili kuwawakilisha watanzania wenzao katika mchakato nyeti wa kutunga Katiba Mpya ambyo ni sheria mama. Hii ni dhamana nyeti, inayopaswa kutekelezwa kwa uadilifu na weledi mkubwa; hekima na unyofu, ili kweli amani, upendo na mshikamano miongoni mwa watanzania uendelee kudumu!







All the contents on this site are copyrighted ©.