2014-04-24 11:18:34

Kuweni macho na watu wanaodai kupigiwa simu na Papa Francisko!


Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa Vatican anafafanua kwamba, katika maisha na utume wake, Baba Mtakatifu Francisko amekuwa akizungumza na watu mbali mbali kwa njia ya simu, kama sehemu ya mkakati wake wa shughuli za kichungaji.

Huu si utume wa Baba Mtakatifu katika maisha ya hadhara, kumbe, Idara ya habari mjini Vatican haina sababu na wala hakuna sababu ya kusubiri maelezo na ufafanuzi wa kina kutoka Vatican kuhusiana na mazungumzo ya simu yanayofanywa na Baba Mtakatifu Francisko.

Padre Lombardi anasema, baadhi ya taarifa zilizosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kinyume kabisa cha matakwa ya mawasiliano kati ya Baba Mtakatifu Francisko na wahusika hazina ukweli wowote, ni habari za kuzusha zinazotaka kuwachanganya watu. Waamini na watu wote wenye mapenzi mema, wanapaswa kuwa makini kuhusiana na habari hizi mintarafu Mafundisho Tanzu ya Kanisa.All the contents on this site are copyrighted ©.