2014-04-19 08:31:26

Wasichana 114 bado wanashikiliwa na Kikundi cha Kigaidi cha Boko Haram


Habari zilizokuwa zimetolewa na Jeshi la Nigeria kwamba, watoto wa shule waliokuwa wametekwa nyara hivi karibuni kutoka shule ya Chibok wameachiliwa huru si za kweli na kwamba, wasichana hao bado wanashikiliwa na Kikundi cha Kigaidi cha Boko Haram, ambacho bado kinaendelea kusababisha majanga makubwa kwa wananchi na mali zao.

Taarifa zinaonesha kwamba, kati ya watoto 115 kati ya wasichana 129 waliokuwa wametekwa hawajulikani mahali alipo. Hayo yamesemwa na Asabe Kwanbura, Mwalimu mkuu wa shule ya wasichana ya Chibok. Ni wasichana 14 tu waliopatikana hadi wakati huu tunapoandika taarifa hii baada ya kuwatoroka watekaji wao na kutokomea msituni. Wasichana wengine 115 bila shaka bado wako mikononi mwa wateka nyara wao.All the contents on this site are copyrighted ©.