2014-04-19 11:14:48

Je uko upande wa Yuda au wa Petro?


Katika historia Takatifu ya ubinadamu wa Yesu wakati wa mateso, mna hadithi nyingi dogondogo kuhusu wanaume na wanawake waonaswa katika hili au kwa kuungana na Yesu katika mateso yake au kuwa wapinzani, kama ilivyokuwa kwa Yuda Iskariote. Na mna mengi ya kutuamiba. Padre Cantalamessa aliianza hivyo tafakari yake ya kipindi cha Pasaka, kwa Papa na wafanyakazi katika majengo ya Vatican,siku ya Ijumaa Kuu.

Alisema, kitendo cha Yuda cha kumsaliti Yesu ni kati ni matukio yanayo ajwa katika Injili zote nne na Agano jipya kwa ujumla. Na Wakristu wa mwanzo walilitafakari hili kwa kina. Nasi pia hatuwezi kukosa kufanya hivyo , katika kipindi hiki cha Mateso ya Yesu, maana mna mengi ya kutueleza.

Yuda Iskarioti ni kati ya Wafuasi wa Yesu waliochaguliwa tangu mwanzo, kuwa mmoja wa wanafunzi wake kumi na wawili . Injili ya Luka ikitaja majina ya mitume , Yuda Iskarioti anatajwa ambaye baadaye alikuwa msaliti (Lk 6:16). Hivyo Yuda hakuzaliwa kama mtoto msaliti na wala hakuwa msaliti wakati Yesu akimchagua, lakini baadaye akawa na moyo huo wa usaliti ! Hili linaonyesha jinsi binadamu alivyo huru mbele ya giza kuu la uhuru wa binadamu.

Padre Cantalamensa amenukuu Maandiko Matakatifu “ Fedha ni chanzo cha uovu na mzizi wa uovu wote". Nyuma ya fedha mna kila ovu linalotokea katika maisha ya kijamii. Ni fedha imehusika kwa namna moja au nyingine .Ni kama ilivyokuwa kwa Moleki tunayemsoma katika Biblia aliyetolea sadaka ya maisha ya wavulana na wasichana ( Yer 32:35 ) au mungu Azteki ambaye alitolewa sadaka kila siku idadi kadhaa ya mioyo ya watu iliyotakiwa. Leo hii ndivyo tunavyoshuhudia miungu wengine wa kidunia kama mapenzi katika biashara ya haramu ya dawa za kulevya inavyo haribu maisha ya watu , au utendaji wa mafia , au kisiasa na nyuma ya uzalishaji mwingi wa silaha na biashara yake, na maovu mengine mengi ambayo yanatisha hata kutaja, mfano mauzo ya viungo vya binadamu vinavyo tolewa kwa watoto , na kipeo cha uchumi tunapopita sasa, sababu kubwa ya uwepo unyama huo ni kwa sababu ya laani ya uroho wa fedha, unaogandamiza watu. Yuda alianza tabia ya kudokoa kidogo kidogo fedha aliyokabidhiwa kutunza, Na hivyo ndivyo inavyotokea hata sasa kwa watawala wengi wa fedha za umma.

Licha ya njia hizi za haramu ya kujipatia fedha , je pia si kashfa kwa baadhi ya watu kupata mishahara na au malipo ya uzeeni ambayo yako juu hata kwa mara mia (100) zaidi kuliko wafanya kazi wa kawaida wanaowasaidia , ambao hupaza sauti zao kudai nyongeza ya mishahara, kw akuwa hawawezi kumudu gharama msingi za maisha? Watu wa kipato cha chini wanaodai uwepo wa uwiano wa haki zaidi katika jamii ?Lakini watu wanapenda kujenga jina lao kwa nguvu ya fedha. Kuwa mtu wa kujulikana kwa sababu ya wingi wa Fedha, kuonea fahali badala ya aibu kuitwa mzee wa fedha, mtu wa fedha !

Kama ilivyo katika miungu wote, fedha ni udanganyifu na uongo, fedha hutoa dhamana bandia katika usalama wa mtu, maana dhamana hiyo huyeyuka mara fedha inapoishia. Hutoa ahadi uhuru na mara huiteketeza.

Na je ni mara ngapi sisi tunafikiria juu ya Mfano uliotolewa na Yesu , wa tajiri aliyefikiri sasa yu salama baada ya kujikusanyia mali nyingi aliyesema "sasa naweza kupumzika na kula maisha", lakini usiku huo, Mungu alimwambia “Mpumbavu ! Usiku huu roho yako itachukuliwa ; Je vitu ulivyo kusanya vitakuwa vya nani? "(Lk 12:20) !

Padre Cantalamensa ameeleza na kuonya Wanaume, kwa wake , wanaokwepa kufuata taratibu zilizowekwa kwa ajili ya kuhifadhi fedha katika benki, badala yake wanakwepa taratibu kwa hongo au kuweka fedha hewa au kuhodhi fedha, wakikwepa ushuru. Watu wanaojikuta na kesi katika mahakama au kufungwa gerezani , kwa uovu kama wa yule tajiri "sasa nimejikusanyia ya kutosha naweza kupumzika", badala yake wanajikuta jela. Je huko jela kuna wakati mzuri? Je , kufungwa huko kwa ajili ya wizi wa fedha za umma ni jambo jema kwa watoto wao na familia zao, huu si ubatili? Kwa nani kufanya hivyo?
Pia tafakari yake imeen delea kuwafikiri watu wanaomsaliti Yesu kwa namna nyingine mbalimbali kwa ajii ya kujipatia vipande 30 vya fedha kama ilivyokuwa kwa Yuda. Mtu anayemsaliti mke wake ,anamsaliti Yesu . Mtumishi wa Mungu asiyekuwa mwaminifu katika ahadi zake ni kumsaliti Yesu na ndivyo ilivyo ktika dhambi zote ni kumsaliti Yesu, Usaliti ni jambo la kutisha.
Sasa je tufanye nini? Kumbeni ni lazima kuchagua kati ya mawili au kumfuata Petro au kuwa upande wa Yuda. Petro alijuta kwa kitendo chake cha kumkana Yesu,lakini maraalitambua kosa lake na kutubu na uendelea kumwamini iYesu kuwa ndiye Kristu na Masiya , nakubaki mfuasi imara wa Yesu. Yuda pia aliona ametenda dhambi na kutoa kilio cha nguvu akisema nimeisaliti damu isiyokuwa na hatia, na kurudisha fedha alizokuwa amelipwa, lakini hakurudi kwa Yesu bali aliishia zake.hakuwa na imani kama Yesu ni Bwna na anaweza kumsamehe dhambi zake. Hivyo tunaiona tofauti ya watu hawa wawili kwamba, Petro alikuwa na Imani katika huruma ya Kristo , lakini Yuda hakuwa hivyo. Yuda baada ya kutenda dhambi usaliti, haonyesha imani katika huruma ya Mungu ya kusamehe dhambi.
Kwa udhaifu wa kibinadamu, nasi pia mara nyingi tunaaguka na kuwa wasaliti kama Yuda. Lakini tusiwe kama yeye, tusiige ukosefu wake wa kutoamini katika msamaha wa dhambi, unaotolewa katika sakramenti ya upatanisho. Sakramenti hii ya ajabu . ! Ni Sakramenti yenye utamu mwingi na uzoefu wa Yesu kama Mwalimu na kama Bwana, na kama mkombozi. Ni sakramenti ya furaha kama ya mtu yule aliye okolewa kutoka katika dimbwi refu, au kama Petro alivyookolewa wakati akididimia baharini. Na kama ilivyokuwa kwa mtu mwenye ukoma aliyepona baada yakiukiri imani kwa Kristo, " Nataka! kuwa safi "(Mt 8:03 ).

Padre Cantalamensa aliendelea kusema, kukiri makosa, kunaturuhusu sisi kuona mafundisho ya kanisa juu ya dhambi ya asili ya Adamu, katika fumbo hili la Pasaka, wakati wa giza la Pasaka linapotoweshwa na mwanga wa Pasaka kwa wimbo Mkuu. Ni kosa la furaha, linalopata utukufu Mkuu wa mkombozi! " Yesu anajua jinsi ya kuchukua dhambi zetu zote, mara moja tunapofanya makosa na kutubu, yanakuwa ni makosa ya furaha, yenye kutukumbusha huruma ya Mungu na unyenyekevu wake mtakatifu.

Padre Cantalamensa alikamilisha tafakari yake akimtakia kila mmoja, ile Siku ya Jumatatu Kuu aamshwe maneno ya muumini mkuu wa nyakati zetu, mtumishi wa Mungu Paul Claudel , katika mioyo yetu:
Mungu wangu , nimehuishwa upya , na sasa ni kijana tena !
Mimi nilikuwa nimelala , kama mtu mfu wakati wa usiku.
Nawe ulisema , na iwe mwanga , na kuamka kwa kilio cha ukelele !
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
Baba yangu, uliyenipa maisha kabla ya alfajiri , ninajiweka katika uwepo wako.
Moyo wangu ni huru na kinywa changu ni safi ; mwili wangu na roho yangu vinafunga.
Nimesamehewa dhambi zangu zote , ambazo nikiri moja baada ya nyingine.
Na sasa pete ya harusi ni juu ya kidole changu na uso wangu umeoshwa.
Mimi ni kama kiumbe asiye na hatia katika neema yako uliyonijalia mimi .

Hivi ndivyo Mateso ya Kristo yanavyo weza kututendea sisi.








All the contents on this site are copyrighted ©.