2014-04-18 10:01:53

Alhamisi Kuu Papa Francisko alihimiza kutumikiana kwa upendo


Katika ishara ya unyenyekevu na huduma, na kwa mwanga wa kumwiga Kristo , Papa Francisko, alivaa dramatic, alama ya huduma na kupiga magoti na kuwaosha miguu wagonjwa 12 katika kituo cha huduma kwa Wagonjwa walemavu cha mjini Roma , wakati akiongoza Ibada ya Alhamisi kuu jioni “ Coena Domini”.
Mapema Alhamisi Papa aliongoza Ibada ya kubariki mafuta ya Mpako wa wokovu “Krisma”, ambayo pia ni ilikuwa ni Siku Kuu ya Mapadre wote. Katika Ibada hii Papa aliwakumbusha Mapadre wote kwamba , kukubali kupakwa mafuta ya kuwa kuhani ni kukubali kuwa mtumishi wa wote na ni zawadi ya utumishi ya kudumu milele. Hivyo Furaha ya upadre haina mwisho , ni zawadi ya uadilifu, uaminifu na utii kwa Bwana.
Na wakati wa Ibada ya Karamu ya mwisho, Papa licha ya kuonekana mchovu, na kusaidiwa kupiga magoti na kusimama, aliongoza liturujia ya kuosha miguu ya wagonjwa 12 waliokuwa wameandaliwa, katika kituo cha kuhudumia wagojwa cha St Maria della Provvidenza Foundation Roma . Kwa huruma na upendo mkuu, Papa alimwendea kila mmoja wao na kumwosha mguu , kuikausha na kisha kuubusu, kama ishara ya sadaka ya upendo na kumtazama usoni kwa makini, kulingana na hali ya afya ya mgonjwa . Wagonjwa hao walikuwa na umri kati ya miaka 16-86 , na wote wanakabiliwa na ulemavu mbalimbali. Wengi walikuwa ni raia wa Italia, watatu wakiwa na asili ya makabila ya mbali mmoja wao akiwa ni Muislim.

Kituo hiki cha Santa Maria della Provvidenza, ni kati ya vituo 12 vya huduma ya afya vinavyoendeshwa Shirika la Don Carlo Gnocchi Foundation. Ibada hii iliweza kutoa tafakari makini katika tabia ya kituo hicho cha afya na kwa Wakristo, wanao fanya kazi ya kujitolea katika kituo hiki cha wagonjwa walemavu, hasa kwa siku za Jumapili ambamo huchanganyika na wagonjwa katika kuadhmisha Ibada ya Misa na kumtukuza Mungu kwa nyimbo . Wengi wa wagonjwa wa kituo hiki ni wagonjwa wasioweza kutembea na hivyo wengi wao hutumia baiskeli za wagonjwa.

Ibada hii ya kukumbuka Karamu ya mwisho ya Bwana na mitume wake , na liturujia kuosha yake ya miguu yao, kama ishara ya huduma, na uzinduzi wa Sakramenti ya Ekaristi , huashiria mwanzo wa kipindi cha Siku Tatu Kuu za Pasaka “ Triduum”.

Uchaguzi wa Papa wa kuadhimisha mwanzo wa Siku Tatu Kuu za Pasaka kwa ishara yake ya kuosha miguu ya watu 12 wenye ulemavu ilikuwa na lengo la kusisitiza aina ya udhaifu, ambayo jumuiya ya Kikristo inaitwa kutambua mateso ya Kristo, ambayo ni lazima kujishughulisha nayo kwa makini , mshikamano na upendo .

Katika hotuba yake fupi , Papa alikumbusha kwamba Mungu alijifanya mtumishi kupitia mwanae Kristo na huu ni urithi wa waamini wote. Kristo alikuja upendo na wafuasi wake wanapasa pia kutoa jibu la upendo la kuwa watumishi katika upendo. Na alizamisha zaidi upendo huo akisema, kuosha miguu ya mwingine, wakati wa Yesu , ilikuwa ni kazi ya mtumwa au mtumishi wa nyumbani. Katika utekelezaji wa ishara hii , Yesu anawaambia wafuasi wake kwamba wao wameitwa kuwa watumishi kwa kila mmoja, hata mtu mdogo sana asiyeonekana kuwa na maana katika jamii.

"Kila mtu hapa lazima kufikiria wengine ... na jinsi ya kuwatumikia wengine kuwa ubora zaidi," alisema .

Huu ni mwaka wa pili Papa kuadhimisha Misa ya Bwana Karamu ya Mwisho kati ya kundi la watu wa kawaida walio tengwa na jamii. Mwaka jana, Papa sherehe Misa ya Bwana Karamu ya Mwisho katika kituo cha Gereza la vijana na watoto watukutu







All the contents on this site are copyrighted ©.