Wasichana 100 kati ya 129 waliokuwa wametekwa nyara waachiwa huru!
Jeshi la Nigeria limefanikiwa kuwaokoa wasichana 100 kati ya 129 wa shule ya sekondari
mjini Borno, Kaskazini mwa Nigeria waliokuwa wametekwa na Kikundi cha kigaidi cha
Boko Haram, mapema juma hili. Taarifa zinaonesha kwamba, wasichana 14 walifanikiwa
kujiokoa wenyewe kwa kuruka kutoka kwenye Lori lilikokuwa limewabeba.
Wasichana
wengine 10 waliweza kutoroka wakiwa msituni, walipokuwa wameambiwa kuwapikia wanajeshi
wa Boko Haram, na kuwaacha bila ya uangalizi makini. Taarifa ya kijeshi iliyotolewa
na Meja Jenerali Chris Olukolade inasema kwamba, mwanajeshi mmoja wa kikundi cha Boko
Haram ametiwa pingu, tayari kufikishwa mbele ya mkondo wa sheria.