2014-04-17 09:41:26

Papa mstaafu Benedikto XVI asherehekea miaka 87 ya kuzaliwa kwake!


Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI, Jumatano tarehe 16 Aprili 2014 ameadhimisha Miaka 87 tangu alipozaliwa, kwa kusali, kutafakari na kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyoweza kumkirimia katika maisha yake hadi wakati huu. Kutokana na Siku hii kuangukia kwenye Juma takatifu, Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita anasema Padre Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican kwamba, ameamua kuiadhimisha katika hali ya utulivu na ukimya pasi na makuu.

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko, Siku ya Jumatano amempigia simu na kuzungumza na Papa mstaafu Benedikto wa kumi na sita, kwa kumtakia heri na baraka anapoadhimisha Siku kuu yake ya kuzaliwa. Anasema amemkumbuka katika sala na sadaka ya Misa Takatifu, Jumatano, kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha, kilichoko mjini Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.