2014-04-16 15:29:45

Majina kadhaa yaidhinishwa na Papa katika mchakato wa utakatifu


Jumanne, Aprili 15, 2014 , Baba Mtakatifu Francisko , alikutana katika hali ya faragha na Kardinali Angelo Amato, Mkuu wa Shirika kwa ajili ya utajaji wenye Heri na Watakatifu. Katika majadiliano yao, Papa alikubali miujiza iliyofanywa na watumishi wa Mungu kadhaa na kuliruhusu Shirika liendelee na Mchakato wa watumishi hao, kutajwa watakatifu.Miujiza iliyokubali na Papa ni:
Muujiza unaohusishwa maombezi ya Mwenyeheri Ludovico ya Casoria , Padre wa Shirika la Ndugu Wadogo na Mwanzilishi wa Usharika wa Masista wa Mtakatifu Francis wa Elisabettine. Alizaliwa Italia, Machi 11, 1814 na kufariki Naples (Italia) Machi 30, 1885.
Pia muujiza wa maombezi ya Mwenye Heri Amato Ronconi , wa Kanuni ya Tatu katika Shirika la la Mtakatifu Francisko ,Mwanzilishi wa Makazi ya mahujaji watu Maskini katika mji wa Saludecio, ambayo sasa ni jengo la mapumziko ya Mwenye Heri Amato Ronconi ; aliye zaliwa Saludecio (Italia) mwaka 1226 na kufariki Rimini (Italia) 1292.
Pia Papa ametambua fadhila ya kishujaa wa Mtumishi wa Mungu Maria Alano de Guynot Boismenu , wa Usharika wa Wamisionari wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, aliyekuwa Askofu Mkuu wa jina wa Claudiopolis , na Mwakilishi Kitume wa Papa wa Papua ; alizaliwa katika Saint- Malo (France) Desemba 27, 1870 na kufariki Kubuna ( Jamhuri ya Visiwa vya Fiji, Oceania) Novemba 5, 1953 ;
Na fadhila kishujaa wa Mtumishi wa Mungu William Janauschek , Padre wa Shirika la Mapadre wa Patakatifu pa Mkombozi; alizaliwa mjini Vienna (Austria) 19 Oktoba 1859 na kufariki Juni 30, 1926 .










All the contents on this site are copyrighted ©.