2014-04-15 13:48:30

Salam na matashi mema kutoka kwa Papa Francisko!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne asubuhi tarehe 15 Aprili 2014 amekutana na kuzungumza na Askofu mstaafu Chabrel Georges Merhi wa Jimbo Katoliki la San Charble en Buenos Aires, Argentina pamoja na Askofu Marcello Semeraro, Katibu mkuu wa Sekretarieti ya Makardinali, kwa pamoja wametembelea ofisi mbali mbali za Sekretarieti ya Vatican ili kusalimiana na viongozi pamoja na wafanyakazi wa Vatican ili kuwapatia kheri na baraka kwa Siku kuu ya Pasaka ya Bwana.

Wafanyakazi wengi walishangazwa kukutana uso kwa uso na Baba Mtakatifu wakati wakiendelea na shughuli zao. Huu ni mwelekeo mpya wa mawasiliano si tu kwa kukutana na makundi makubwa ya watu, bali kila mtu anayo nafasi katika maisha na utume wa Baba Mtakatifu Francisko. Wafanyakazi wamefurahi, kwani si rahisi baadhi yao kukutana na Baba Mtakatifu mara kwa mara kutokana na aina ya kazi walizo nazo!All the contents on this site are copyrighted ©.