2014-04-15 09:20:33

Papa atoa zawadi ya Injili kwa wafungwa


Papa Francisko atatoa vitabu vya Injili vidogo vinavyoweza kuwekwa mfukoni, vipatavyo elfu moja mia mbili, kama zawadi ya Pasaka kwa wafungwa katika Gereza Kuu la Malkia wa Mbingu la Roma. Zawadi ya Papa itawasilishwa Jumatano hii, na Askofu Mkuu Konrad Krajewski wakati atakapo tembelea jengo la Gereza katika mtaa wa Lugara Roma.

Kitabu hicho kidogo cha Injili chenye kuwa pia waraka wa Matendo ya Mitume, Jumapili iliyopita pia kiligawiwa kwa waamini waliofika kumsikiliza Papa wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, na pia kwa waliohudhuria Ibada ya Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu George Mkuu la Magliana Roma.

Na Jumapili ya tarehe 4 Mei, Papa ana mpango wa kufanya ziara ya Kichungaji katika Kanisa la Mtakatifu Stanslao la Botteghe la Roma.
Kisha 18 Mei 2014 , majira ya saa kumi za jioni , Papa Francesko atafanya hija katika Madhabahu ya Bikira Maria wa Upendo wa Mungu, ambayo yako katika Mtaa wa Via Ardeatina nell’Angola Romano , nje kidogo ya jiji la Roma. Hija inayopendwa na watu wa Roma.

Madhabau ya Bikira Maria wa upendo wa Mungu, ya Mtaa wa Via Ardeatina , yako kiasi cha umbali wa kilomita 12 Roma, katika kanda ya Agro Romano katika jengo la Castel di Leva. ambalo kwa mara ya kwanza liliteuliwa na Papa Gregoria V11 kwa barua yake ya kitume ya mwaka 1081, kama mali ya Abassia ya Mtume Paulo . Na mwaka 1268, mali hiyo ililithishwa kwa Kanisa la Mtakatifu Sabina na baadaye kupewa Wana shirika wa Orsinina mwaka 1295na tena kuhamishiwa kwa Wasaveli.
Na baada ya kupitia katika mbadiliko mbalimbali, Desemba 1938, Madhabahu hayo yalifanywa kuwa Parokia ikiongozwa na Paroko wa kwanza Don Umberto Terenzi ambaye mwaka 1942 alianzisha Shirika la Mabinti wa Maria wa Upendo wa Mungu na mwaka 1962, madhabahu hayo yakawekwa chini ya usimamizi wa Shirika la Oblates hadi leo.
Simulizi juu ya madhabahu hayo, huelezea tukio la mwaka 1740, juu ya muujiza uliotokea kwa muhujaji mmoja aliyekuwa akisafiri kwenda Roma kuhiji ambaye alipofika katika eneo hilo, kulitokea kundi la mbwa mwitu wakali walotaka kushambulia, lakini mara aliomba msaada wa Mama Bikira Maria na ghafla mbwa wao walizuiwa na kitu kisichoonekana na kutoweka zao. Aidha watu wa Roma wanasadiki, Sanamu ya Bikira Maria wa Upendo wa Mungu iliyo katika eneo hili iliweza kuuokoa mji wa Roma dhidi ya kuanguka katika mikono ya maadui wakati wa vita kuu ya pili ya dunia.


Ushuhuda wa kuokelewa na Bikira Maria wa Upendo wa Mungu, ndiyo asili ya hija katika eneo hili ambako waamini wanapenda kwenda kuomba msaada wa kwa Bikira Maria kutatua shida zao mbalimbali na pia kwa ajili ya kutoa shukurani zao kwa mambo mbalimbali waliyofanikisha.







All the contents on this site are copyrighted ©.