2014-04-14 15:04:34

Wakristu wameanza kipindi cha Juma Takatifu


Katika Jumatatu hii ambayo ni siku ya kwanza katika Juma Takatifu, Baba Mtakatifu Francisko, amelifungua Juma kwa kukutana na Kardinali Leonardo Sandri, Mkuu wa Shirika kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki. Na pia amekutana na Kardinali Agostino Vallini, Vika Mkuu wa Jimbo la Roma, na baadaye majira ya saa sita alikutana na Jumuia ya Chuo cha Kipapa cha Leoniano di Anagni, katika ukumbi wa Clementina mjini Vatican.
Hotuba ya Papa kwa Maaskofu , Mapadre na Waseminaristi wa Chuo cha Kipapa cha Leoniano di Anagni, kwa namna ya kipekee, ulianza na kutoa salaam maalum kwa waseminaristi ambao wamefanya hija ya kutembea kwa miguu kutoka chuoni hadi Roma. Papa amesema ni ishara inayonyesha ujasiri na kukua katika safari yao na mwamko wa kusonga mbele kwa shauku kubwa, uvumilivu, upendo wa Kristo na ushirika na wengine.

Papa alionyesha kutambua umuhimu wa seminari ya Leonian di Anagni, ambayo hutoa huduma kadhaa katika mkoa wa Lazio Italia, akisema inaendeleza utume wake wa tangu kale, kuwapokea walioitwa na kanisa, kwa ajili ya kuyashiriki majiundo na uzoefu hadi kuwa kuhani, mwenye kutoa matunda ya kweli ya kitume. Na kama ilivyo kwa kila seminari, lengo likiwa kuwaandaa wachungaji wa baadaye, walioteuliwa kupitia mazingira ya maombi, kujifunza na maisha ya pamoja katika ushirika. Ni katika hali hiyo ya kiinjili, maisha haya yaliyo jaa Roho Mtakatifu na ya ubinadamu, huendelea kuwepo na kuzama kwa watu wengi siku hadi siku katika hisia za utendaji wa Yesu Kristo na upendo wake kwa Baba na kwa Kanisa, kujitolea kwake bila ya kujibakiza kwa Watu wa Mungu

Papa alimewasihi Wasemanaristi wayapokee maisha ya kitawa kwa uelewa mkubwa na uvumilivu mwingi kama wanavyojifunza wakati wa maandalizi yao ya kuwa wahudumu na maafisa wa chombo chenye kuwa na urasimu mwingi. Aliwahimiza wawe makini, na wasianguke kwa hili! Na wachaguae kuwa wachungaji wa kweli katika sura ya Yesu Mchungaji Mwema, kwa kuwa yeye mwenyewe binafsi daima yu kati ya kundi lake , akiwalisha kondoo wake.

Mbele ya changamoto inayokabili wito wao, wanaweza kutoa jibu kama Mama Bikira Maria malaika kwa Malaika Je, inawezekana Jambo hili? (Taz. Lk 01:34 ). Kuwa wachungaji wema katika sura ya Yesu ni kitu kikubwa sana, na wao ni watu wandogo sana mbele ya hilo... Lakini pamoja na ukweli huo, hakuna cha kuongopa maana si kazi yao . Ni kazi ya Roho Mtakatifu inayofanikishwa kwa pamoja na ushirikiano wao. HIvyo inakuwa ni jambo la kujitoa kwa unyenyekevu, na kukubali kufinyangwa kama ilivyo udogo mbichi mbele ya mfinyaji anapotaka kuunda chungu.
Mfinyanzi huyo ni Mungu , kazi na maji na moto , ni Neno na Roho Mtakatifu . Ni kuyameza na kuyaishi maneno ya Mtume Paulo aliye sema, " si mimi tena, bali Kristo anaishi ndani yangu" ( Gal 2:20). Hii ina maana maana kutafakari injili kila siku , na kuiishi na kuhubiri ; maana ya uzoefu katika huruma ya Mungu inayopatikana katika sakramenti ya Upatanisho. Ni kuwa watumishi karimu na wenye huruma; ni kujilisha imani na upendo wa Ekaristi, kulisha Wakristo; maana ya kuwa watu wa maombi ,sauti ya Kristo, katika kumtolea sifa, utukufu Baba wa Mbinguni na maombezi kwa ajili ya ndugu zetu. (taz.Ebr 7:25).
Papa amewaasa wasseminaristi hao kufanya uchaguzi thabiti wa njia y amaisha ya Kikristo, kwa kuwa kuna njia nyingi katika safari na uzoefu wa maisha ya binadamu. Alisema, Iwapo kuna anayeona njia hii ya ukuhani haimfai tena, kuziishi sheria na kanuni zake,si vibaya kuamua kwa ujasiri kuachana nayo na kuchagua njia nyingine. Kuna njia nyingi , katika Kanisa , kwa ajili ya kuishi na kumshuhudia Kristo. Katika njia ya kuwa mfuasi wa Yesu katika ukuhani wake, daima ni kukubali kuongozwa na mifano mingi ya maisha yaa watu Watakatifu wa Mungu waliyo yatolea maisha yao kikamilifu si kwa faida zao wenyewe lakini kwa faida ya binadamu wengine. Papa ameonya kwa kutumia Maandiko Matakatifu, "Ole wao wachungaji waovu ambao hujichunga kwa manufaa yao wenyewe na si kundi"! Nabii (cf. Ez 34.1-6 ). "Ole wao wanaofikiri tu juu ya faida na maisha yao ya baadaye".

Papa alimalizia kwa kutoa shukurani zake za dhati kwa ziara yao. Na kwamba atawasindikiza nakuongozana nao kupitia njia ya maombi na sala, na aliwabariki na kuwakabidhi kwa Bikira Mama, na pia aliomba maombezi yao.








All the contents on this site are copyrighted ©.