2014-04-14 15:37:16

Rambi rambi za Papa kwa janga la moto Valparaiso Chile.


Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican amepeleka salaam za rambirambi za Papa Francisko, kwa njia ya telegram kwa Askofu Gonzalo Duarte Garcia De Cortàzar wa Jimbo la Valparaíso, kufuatia tukio la kusikitisha na moto mkubwa kukuba mji wa Valparaiso.
Papa Francisko, mara baada ya kusikia habari ya kusikitisha ya moto wa kutisha kutokea katika mji wa Valparaíso, ameonyesha ukaribu wake wa kiroho kwa wakazi wa mji huo, kwa matoleo ya sadaka ya sala kwa wote walio athirika katika janga hili na kubwa, akishirikishana uchungu na majonzi ya wale ambao wamepoteza jamaa, makazi na mali zao.
Pia Papa anawakumbuka katika sala zake, kikosi cha uokoaji , pamoja na mamlaka ya utawala wa jiji na watoaji wa huduma zote za msaada wa kibinadamu, unaotolewa katika hali ya udugu na mshikamano kwa ajili ya watu wote, ili kwamba wasipoteze moyo wa matumaini katika uso wa mashaka.

Pia Papa amepeleka salaam za rambirambi kwa wafiwa wote. Kwa hisia hizo , Papa anawapa baraka zake maalum za kitume kama ishara ya upendo kwa Wachile wote.








All the contents on this site are copyrighted ©.