2014-04-12 12:05:36

Professa Margaret Scotford Archer, ateuliwa kuwa ni Rais Baraza la Kipapa la Taasisi za sayansi Jamii


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Professa Margaret Scotford Archer, kuwa Rais wa Baraza la Kipapa la Taasisi za Sayansi Jamii. Professa Archer alizaliwa tarehe 20 Januari 1943. Baada ya masomo yake kwa miaka mingi alikuwa ni Jaalimu wa Sayansi Jamii nchini Uswiss. Kunako tarehe 19 Januari 1994 akateuliwa na Mwenyeheri Yohane Paulo II kuwa mjumbe na muasisi wa tume hii.

Professa Archer ni mtafiti katika nyanja za Falsafa Jamii pamoja na Nadharia za Kijamii. Ni mwandishi mashuhuri wa vitabu na majarida mbali mbali duniani.







All the contents on this site are copyrighted ©.